Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Faida ya sarafu moja Afrika Mashariki

Faida ya sarafu moja Afrika Mashariki

0 comment 94 views

Imeshuhudiwa nchi wanachama wa jumuiya mbalimbali ikiwemo Ulaya wakichukua hatua kadhaa katika kuimarisha uchumi wa nchi mwanachama kwa kuanzisha sarafu moja yenye kutumika katika nchi zote mwanachama wa umuiya hiyo.

Moja ya sarafu zilizofanikiwa katika jumuiya mbalimbali duniani ni pamoja na sarafu ya Euro ambayo imekuwa ikitumika bara la Ulaya katika nchi mwanachama ili kuhakikisha lengo la kukuza uchumi kwa wanachama kupitia shughui za kibiashara, uwekezaji na uchukuzi zinafanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Hivi sasa kuna mchakato wa kuanzisha sarafu moja kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mchakato wa kuanzisha umoja wa fedha unaolenga kuanzishwa kwa sarafu moja kwa nchi za wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulianza  Januari 2011 wakati majadiliano kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuandaa itifaki ya kuanzisha umoja wa fedha yalipoanza rasmi. Majadiliano hayo yalikamilika mwezi Julai 2013 na itifaki ya kuanzisha umoja wa fedha kupitishwa na Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki Novemba 2013 katika mkutano wa 15 wa wakuu hao uliofanyika jijini Kampala.

Ili kutimiza dhumuni kuu la umoja wa fedha la kujenga ukanda tulivu wa kifedha utakaorahisisha na kusaidia ukuaji wa biashara. Hata hivyo mchakato huu wa kuanzisha sarafu moja unatarajiwa kuanzishwa mara baada ya itifaki hiyo kuridhiwa na mabunge ya nchi wanachama wa jumuiya.

Faida itakayopata Tanzania kutokana na umoja wa fedha na hasa kuwepo kwa sarafu moja ya jumuiya ya Afrika Mashariki ni pamoja na;

  1. Kupunguza gharama za kufanya biashara katika nchi wanachama na hivyo kuhamasisha ukuaji wa biashara kati ya nchi wanachama na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.
  2. Kwa kuwa na sarafu moja, umoja wa fedha utaepusha athari za ubadilishaji wa fedha ndani ya jumuiya.
  3. Kuwezesha nchi wanachama kuwa na kiwango kidogo na tulivu cha mfumuko wa bei.
  4. Kuwezesha nchi wanachama kuwa na viwango vidogo vya riba vya kukopa.
  5. Kutumia sarafu moja kutaleta uwazi katika bei na hivyo kuongeza ushindani wa soko ndani ya jumuiya.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter