Home FEDHA Bajeti kuu ya serikali kujulikana leo

Bajeti kuu ya serikali kujulikana leo

0 comment 104 views

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango anatarajia kuwasilisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019 leo bungeni Dodoma ikiwa ni bajeti ya tatu chini ya utawala wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli. Baadhi ya wabunge wameeleza matarajio yao na kusema kuwa wanategemea bajeti hiyo itazingatia maisha ya wananchi wa kawaida na kupunguza ada, kodi na tozo mbalimbali zilizopo hivi sasa.

Akitoa maoni yake, Mbunge wa Rufiji kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mohamed Mchengerwa amesema  kupitia bajeti hiyo, serikali inapaswa kutekeleza ahadi zilizotolewa kwa wananchi na kuelekeza nguvu zaidi katika kuboresha mazingira ya miundombinu ya umeme. Kwa upande wake, Mbunge wa Vinjo kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia amesema watanzania walio wengi wamekata tamaa na wanapaswa kupewa matumaini ya kuishi kwani wanalia na hali ngumu ya maisha. Ameongeza kuwa, anatarajia bajeti hiyo itakuwa mwanga wa matumaini hasa kwa walipakodi na itaonyesha maendeleo ya watu na sio vitu.

Naye Hussein Bashe, Mbunge wa CCM Nzega Mjini amesema serikali imekuwa ikibana matumizi na  kukusanya kodi kwa takribani miaka miwili sasa hivyo anatarajia bajeti itakayosomwa itachochea uzalishaji na sio kuangazia masuala ya kodi pekee.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter