Home BENKI Azania yasherekea mafanikio na jamii

Azania yasherekea mafanikio na jamii

0 comment 66 views

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara kutoka Benki ya Azania Rhimo Nyansaho amesema siri ya mafanikio ya kiuchumi ya benki hiyo ni huduma bora na kujali wateja. Akiwa kwenye hafla maalum ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja pamoja na jamii yenye uhitaji, Nyansaho ameeleza kuwa benki ya Azania inaendelea kupata mafanikio kutokana na wateja ambao wamekuwa waaminifu kwa taasisi hiyo.

Mmoja kati ya wawakilishi wa wateja aliyekuwepo katika hafla hiyo, Deogratius Kifunani ametoa pongezi kwa benki hiyo kwa huduma zao pamoja na kurudisha sehemu ya mapato yao kwa jamii inayowazunguka.

Katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan benki ya Azania imeamua kufuturisha wateja wa benki hiyo pamoja na watoto yatima kutoka kituo cha Ijango Zaidi kilichopo Sinza jijini Dar es salaam kama sehemu mojawapo ya kushirikiana na jamii katika masuala mbalimbali.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter