Home FEDHABIMA Mauzo bima yapanda 23%

Mauzo bima yapanda 23%

0 comment 109 views

Kamishna wa Bima wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Dk. Baghayo Saqware, amesema mauzo ya bima yameongezeka kwa asilimia 23 na sekta ya bima kwa ujumla imekua kwa asilimia 10 tangu kuwepo kwa Sheria inayowaelekeza waingizaji wa mizigo nchini kukata bima zao katika kampuni zilizo nchini na sio za nje.

“Kwanza ukubwa wa sekta ya bima umekua, bima zote zimekua kwa wastani wa asilimia kumi kuanzia Januari 2018 hadi Septemba 30 mwaka jana na hii ni kwa takwimu tulizonazo na bima hiyo ya uingizaji mizigo imekua kwa asilimia 23”. Amesema Kamishna huyo.

Pia ameongeza kuwa Sheria hiyo imekuwa na manufaa hasa katika pato la taifa kwani kabla, waingizaji wa mizigo nchini walikuwa wanawafaidisha nchi za nje kiuchumi, ingawa pale inapotokea kampuni za ndani hazina uwezo wa kukatia bima mzigo uliozidi, muingizaji wa mzigo huo ataruhusiwa kwa ruhusa maalum kukata bima nje ya nchi.

Dk. Baghayo amehakikisha kuwa hakuna makosa yeyote yatakayotokea pale mauzo na manunuzi ya bima yanapofanyika kwani mamlaka hiyo inamruhusu mteja kulipia kwa njia ya mtandao. Hata hivyo, wale wanaopeleka mizigo nje ya nchi wanaruhusiwa kununua bima zao popote na Kamishna huyo amewasisitiza kununua bima nchini ili kuchangia katika pato la taifa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter