Home FEDHA Deni la Serikali lafika Sh 69.44 trilioni

Deni la Serikali lafika Sh 69.44 trilioni

0 comment 111 views

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia Aprili 2022, deni la Serikali lilikuwa Sh69.44 trilioni ikilinganishwa na Sh60.72 trilioni kwa kipindi kama hicho mwaka 2021, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 14.4.

Kati ya kiasi hicho, deni la ndani Sh22.37 trilioni na la nje ni Sh47.07 trilioni.

Dk Nchemba amebainisha hayo Juni 14, 2022 wakati akiwasilisha hali ya uchumi wa Taifa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2022/23 Bungeni jijini Dodoma.

Amesema taarifa ya tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Novemba 2021 inaonesha kuwa deni la Serikali bado ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu kwa kuzingatia ukomo wa viashiria vyote vinavyokubalika kimataifa.

Dk Nchemba, anatarajiwa kuwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Bungeni jijini Dodoma jioni ya leo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter