Home FEDHA Fanya hivi kupunguza gharama za uendeshaji

Fanya hivi kupunguza gharama za uendeshaji

0 comment 99 views

Siku zote ni muhimu kurahisisha ufanisi wa kazi ili mambo yafanyike kwa haraka zaidi bila kupoteza muda, hii ni kama kampuni inafanya vizuri. Vilevile ni kawaida kwa kampuni kupitia kipindi ambacho fedha inakuwa ngumu au mauzo yanakuwa hayalingani na matumizi. Ikiwa hali hiyo imetokea ni muhimu kwa wamiliki kufanya baadhi ya mabadiliko ili kuhakikisha gharama zinapungua ili kukabiliana na hali iliyopo. Pia kupunguza gharama za matumizi kutasaidia faida kuongezeka.

Kwa kufanya mambo yafuatayo, gharama zitapungua katika kampuni/biashara.

Pitia orodha ya matumizi

Ikiwa kampuni inafanya vizuri ni rahisi kuwa na matumizi ambayo si ya muhimu katika kampuni, lakini ukiwa unataka kupunguza gharama za matumizi ni muhimu kupitia kumbukumbu ya matumizi yote na kuondoa matumizi yasiyo ya muhimu ili kwenda sawa na hali halisi ya kifedha. Kwa mfano badala ya kutumia intaneti ya kasi ambayo inauzwa bei ghali unaweza kubadilisha na kutumia intaneti ya kawaida.

Uzalishaji

Uzalishaji ni muhimu katika biashara. Ikiwa kuna ulazima wa kupunguza gharama za matumizi ni muhimu kuhakikisha mchakato wa uzalishaji hautumii fedha nyingi. Kwa mfano badala ya kutumia umeme kufanya uzalishaji kampuni inaweza kutumia gesi asilia au umeme wa jua ili kupunguza gharama.

Ajira

Mtandao unazidi kurahisisha masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na ajira. Ikiwa kampuni haiwezi kumudu kuajiri watu moja kwa moja na inapitia changamoto katika masuala ya kifedha ni vyema kwa kampuni kuajiri watu kwa kupitia mtandao ili kurahisisha malipo kwa kuwa wafanyakazi wa mtandaoni hulipwa malipo baada ya kazi  na huwa hakuna malipo ya ziada. Kuajiri moja kwa moja huja na gharama mbalimbali kama vile malipo ya likizo, bima, vocha za mwezi, mafuta ya gari nk.

Vifaa

Ikiwa kuna vifaa visivyotumika, sio vibaya kuuza vifaa hivyo ili kuelekeza fedha hizo sehemu zinazohitajika zaidi ili  kuisaidia kampuni.

Tumia mtandao

Siku hizi kuna mitandao mbalimbali ambayo ni rahisi kujitangaza na kupata wateja wengi. Hivyo badala ya kutumia gharama kujitangaza unaweza kujitangaza katika mtandao ya kijamii na kujipatia wateja zaidi.

Nunua kwa bei ya jumla

Kufanya manunuzi kwa bei ya reja reja husababisha gharama kuwa kubwa, hivyo ili kupunguza gharama za matumizi ni vyema kufanya manunuzi ya bei ya jumla.

Likizo

Ikiwa kampuni hutoa likizo zenye malipo, si vibaya kuwajulisha wafanyakazi kuwa wanaweza kuchukua likizo bila malipo hii itakusaidia kupunguza gharama kwa namna moja au nyingine kwa sababu kwanza watakuwa hawapo kazini na pili hata wakiwa likizo kampuni inaepukana na gharama kulipa wafanyakazi wakiwa likizo.

Ni vyema kwa kampuni kuwa na mipango madhubuti kuhusu changamoto zinazoweza kutokea na kuathiri hali ya kifedha. Athari za kifedha huathiri kampuni nzima na wakati mwingine hupelekea hata kupunguza wafanyakazi na kusababisha ongezeko la watu wasio na kazi mtaani jambo ambalo si zuri katika taifa lenye malengo ya kuendelea kiuchumi.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter