Home FEDHA Halmashauri 12 zalamba mabilioni

Halmashauri 12 zalamba mabilioni

0 comment 103 views

Wizara ya Fedha na Mipango imetoa ruzuku ya Sh. 137 bilioni kwa Halmashauri 12 nchini ili kutekeleza miradi 15 ya kimkakati, itakayowezesha Halmashauri hizo kuongeza mapato ya ndani na kupunguza utegemezi wa kibajeti kutoka serikali kuu. Hafla ya uwekaji wa saini kati ya Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa serikali, Dotto James  na Wakurugenzi wa Halmashauri imefanyika Jijini Dodoma na kushuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Dk. Doroth Gwajina pamoja na baadhi ya makatibu tawala wa mikoa ambayo Halmashauri zimepatiwa ruzuku hiyo.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa Halmashauri  zilizopata fedha hizo kuzitumia fedha kwa malengo yaliyokusudiwa, na kutoa onyo kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokiuka makubaliano.

“Maafisa Masuuli mhakikishe mnafuata na kuzingatia Sheria ya Bajeti Namba 11 ya mwaka 2015 na kanuni zake, ambayo pamoja na mambo mengine inasisitiza juu ya matumizi bora ya fedha kwa shughuli zilizoidhinishwa”. Amesisitiza.

Kwa upande wake, Dk. Gwajima kutoka TAMISEMI ameipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kwa upatikanaji wa fedha ambazo amesema zitachochea miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini na kuzitaka Halmashauri zilizosaini mikataba kuzingatia malengo na kutekeleza miradi kwa muda na katika viwango vinavyokubalika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter