Home FEDHAHISA PATA KUFAHAMU KUHUSU HISA

PATA KUFAHAMU KUHUSU HISA

0 comment 127 views

Watu wengi wamekuwa wakitamani kuanzisha biashara na wengine wakathubutu kabisa kuanzisha biashara ila kwa namna moja au nyingine wameshindwa kuendelea na biashara.

Kuna sababu nyingi zilizopelekea kushindwa kwa biashara ikiwapo suala la muda wa kusimamia biashara na changamoto nyingine,

Je , ulishawahi kufikilia kuhusu biashara ya Hisa? Biashara ya hisa ni miongoni mwa biashara ambazo hutumia muda mchache kusimamia.

HISA NI NINI? Hili ni swali ambalo watu wengi hujiuliza.

Kwa kifupi Hisa ni Umiliki. Ukisikia mtu anahisa kwenye kampuni flani, maana yake mtu huyo anakuwa sehemu ya umiliki wa kampuni hiyo.

Mfano kampuni inaweza kuwa na jumla ya hisa 100 wakauza hisa 50 kwenye soko la hisa na kubakiwa na hisa 50, hisa zinaweza kununuliwa na mtu yeyote kulingana na sera ya kampuni husika. Mtu mwenye hisa huwa na nguvu na maamuzi katika kampuni husika.

ADVERTISEMENT

Hisa zinaweza kununuliwa kwenye kwenye soko la Awali (primary market) au soko la pili (secondary market)

Soko la Awali (Primary market)  sehemu ambayo hisa huuzwa/hununuliwa kwa mala ya kwanza kabisa ni kipindi ambacho kampuni inahitaji pesa kwa ajili ya kuongezea mtaji wake. Hapa kampuni huamua ni share ngapi waziuze kwa jamii na pia waziuze kwa bei gani ambayo itawavutia wanunuzi wengi.

Soko la pili (Secondary market) hili ni soko ambalo zile hisa zilizouzwa kwenye primary market  ndio huuzwa au kununuliwa upya.

Kwenye secondary market ndio tunaweza kuona bei za hisa zikipanda au kushukua kutegemea mahitaji ya wanunuzi na wauzaji, kama wanunuzi wakiwa wengi zaidi ya wauzaji husababisha hisa kuuzwa bei kubwa kidogo. Pia kama wanunuzi wakiwa wachache zaidi ya wauzaji bei za hisa husika zitauzwa kwa bei ya chini.

Usikose kusoma chapisho lijaro tutatuzungumzia kuhusu, hali zinazoweza kusababisha hisa kupanda bei au kushuka bei. Pia tutaelezea kuhusu faida na hasara za hisa.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter