Home FEDHA Makusanyo Wizara ya Madini yapongezwa

Makusanyo Wizara ya Madini yapongezwa

0 comment 102 views

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeitoa pongezi kwa Wizara ya Madini kwa ukusanyaji maduhuli, ambapo ndani ya kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2018/19, yaani kuanzia mwezi Julai hadi 31 Desemba, 2018, Sh. 167,742,947,332 zimekusanywa kati ya Sh. 310,598,007,000 iliyopangiwa. 

Akiwasilisha taarifa kwa niaba ya Katibu Mkuu, Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa ameeleza kuwa, Sh. 310,320,004,000 zilipangwa kukusanywa kupitia Tume ya Madini, na Sh. 278,003, 000 katika Makao Makuu ya Wizara na Chuo cha Madini Dodoma. 


“Mhe. Mwenyekiti, hivyo lengo la makusanyo kwa kipindi cha nusu mwaka Julai hadi Desemba 2018 ni Sh. 155,299,003,500. Hadi kufikia tarehe 31 Desemba 2018, Wizara ilifanikiwa kukusanya kiasi cha Sh. 167,742,947,332 sawa na asilimia 108.01 ya lengo”. Ameeleza Kamishna Mulabwa.

Akizungumzia jitihada za Wizara hiyo kuvutia wawekezaji, Mulebwa amesema wizara iliandaa kongamano la kutangaza fursa za uwekezaji katika sekta ya madini nchini lililojulikana kama China Tanzania Mining Forum, lengo kuu la kuongamano hilo likiwa kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini, ikiwemo kutafuta soko la madini nchini China na kuangalia fursa za ushirikiano kati ya Wizara ya Madini Tanzania na Wizara ya maliasili ya China. 

“Mhe. Mwenyekiti kongamano hilo pia lilitumika kuwakutanisha wachimbaji wa Tanzania na watengenezaji wa mitambo mbalimbali ambayo hutumika kwenye shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini”. Amesema

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter