Kuna msemo usemao ‘pesa ni sabuni ya roho’. Watu hufanya kila jitihada kuzitafuta fedha ili waweze kufurahia maisha. Hakuna fedha halali zinazopatikana kwa haraka au bila kufanya kazi kwa bidii na ndio maana watu wasiopenda kujishughulisha hutafuta njia zisizo halali ili kujipatia fedha nyingi kwa haraka.
Hivyo yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo ulikuwa hujui kuhusu fedha
- Kabla fedha hazijaanza kutengenezwa kwa karatasi na sarafu, watu walitumia ndovu, udongo, wanyama, nafaka, vifuko vya ndovu kama fedha. Vitu hivyo vilikuwa havipatikani kwa urahisi na vilikuwa vinatumika kama fedha kwa ajili ya kununua au kuuza bidhaa au huduma.
- Benki za kwanza zilikuwa katika mahekalu ya kidini kwa sababu kulikuwa na ulinzi mkali.
- Inasemekana kuwa takribani ya asilimia 94 ya fedha za karatasi ambazo hupita katika mikono mbalimbali huwa zimejaa bakteria. Uchunguzi uliofanywa na NYU uligundua aina 3,000 za viumbe kwenye bili za dola 80 tu ikiwa ni pamoja na bakteria za nyumonia, sumu ya chakula na hata maambukizi ya staph.
- Inaelezwa kuwa ni asilimia 8 tu ya fedha zote duniani ndio zipo katika mfumo wa sarafu na karatasi (keshi). Hili linaweza kuwa sio jambo la kushangaza sana hasa kutokana na utandawazi na matumizi ya teknolojia zilizoendelea hususani katika kuhifadhi fedha hivyo hakuna umuhimu wa kutembea na fedha kila wakati.
- Inasemekana muuzaji maarufu wa madawa ya kulevya Pablo Escobar alikuwa ana fedha za ziada nyingi sana kiasi kwamba alipoteza kiasi cha dola bilioni 2.1 kwa panya ambao walizitafuna fedha hizo. Escobar alikuwa ameweka fedha katika ghala (warehouse) na kila mwaka alipoteza asilimia 10 ya fedha hizo kutokana na panya.
- Muswada mkubwa uliowahi kuchapishwa na ofisi ya kuchapisha fedha ya Engraving ulikuwa ni wa bili ya dola 100,000 yenye cheti cha dhahabu mwaka 1934 na 1935. Bili hiyo ilikuwa inatumika na hasa na mabenki na mara nyingi haikuonekana kwenye umma. Leo dola 100 ndio muswada mkubwa katika mzunguko wa fedha.
- Kama una dola 20 mfukoni na huna madeni basi unaweza kuwa tajiri zaidi ya asilimia 20 ya wamarekani wengi kwa sababu asilimia kubwa ya watu wanajiendesha kutokana na madeni.
- Mashine ya kwanza ya kutolea fedha (ATM) ilikuwa katika benki ya Barclays huko London mwaka 1967. Ilianzishwa na John Shepherd Barron na watumiaji wa mashine hiyo hawakulipa ada.
- Fedha za karatasi za Marekani si karatasi kabisa: asilimia 75 ni pamba na asilimia 25 ni Enzi za Ben Franklin watu walirekebisha bili zilizochanika kwa kushona na uzi.
- Kuna trilioni za kimarekani 75 dunia nzima. Fedha hizo zikigawanywa duniani kote, kila mtu atapata si chini ya dola 11,000