Home FEDHAMIKOPO Mamilioni yatolewa kwa wanawake, vijana Iringa

Mamilioni yatolewa kwa wanawake, vijana Iringa

0 comment 130 views

Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imetoa mikopo yenye thamani ya Sh. 110 milioni kwa vikundi mbalimbali vikiwemo vya wanawake, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali ambalo limezitaka Halmashauri zote hapa nchini kutenge asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya wanawake, vijana na watu walio na ulemavu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo, Aloyce Kwezi Mwakilishi wake, Dk. John Mwingira amesema wilaya hiyo inatambua mchango mkubwa wa wanawake wajasiliamali hivyo wametumia siku ya wanawake kuwawezesha kujikwamua kiuchumi. Imeelezwa kuwa mikopo iliyotolewa kwa wanawake ni mikopo isiyo na riba na wakopaji hao watatakiwa kurejesha mikopo hiyo kwa muda uliopangwa pasipo kutozwa riba yoyote huku wakisisitizwa kuwa mikopo hiyo inaporejeshwa kwa wakati, vikundi vingine navyo vitanufaika.

“Halmashauri kupitia makusanyo ya mapato ya ndani imeendelea kutekeleza agizo la serikali lililotolewa na Rais Dk. John Magufuli kwa Halmashauri zote nchini kupitia makusanyo yake ya ndani kutenga asilimia 10 kwa ajili ya  kuwakopesha vikundi vya wanawake, walemavu na vijana na Halmashauri yetu imekuwa ikitekeleza kwa vitendo na kwa wakati agizo hilo”. Amesema Dk. Mwingira.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter