Home FEDHAMIKOPO Wanawake wasisitizwa kurejesha mikopo

Wanawake wasisitizwa kurejesha mikopo

0 comment 124 views

Wanawake waliojiunga katika vikundi vya kuweka na kukopa (VICOBA) wameshauriwa kujenga nidhamu ya kurejesha fedha pindi wanapokopeshwa na Halmashauri ili fedha hizo zitumike kusaidia watu wengine kupitia vikundi hivyo. Wito huo umetolewa na Mwanandani Mtonji kwa niaba ya Mkurugenzi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA), Joyce Msiru wakati wa uzinduzi wa kikundi cha VICOBA cha Fiti.

Mtonji amesema kuwa wanawake katika vikundi hivvyo wanapaswa kutumia fedha wanazopata kwa makini ili kuwa na uwezo wa kurejesha fedha hizo kwa wakati.

“Tunatambua Halmashauri zinatoa mikopo katika vikundi vya wanawake hivyo mnapaswa kuwa makini na fedha hizo ili muweze kuzirejesha ili ziweze kuwanufaisha watu wengine na hili litawezekana pale tutakapokuwa na matumizi sahihi ya pesa”. Amesmea Mtonji.

Pamoja na hayo, pia amewataka wanawake kutambua mchango mkubwa walionao katika familia na jamii kwa ujumla huku akiwasisitiza wasirudi nyuma.

“Wanawake ni watu muhimu katika kuleta maendeleo kwa jamii hususani familia inayokuzunguka hivyo tutumie vikundi hivi katika kuleta maendeleo hayo kwa kukopeshana fedha kwa lengo la kupata mitaji ya biashara”. Ameeleza Mtonji.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter