Home FEDHA Njia 4 za kuingiza mkwanja chapchap

Njia 4 za kuingiza mkwanja chapchap

0 comment 124 views

Kadri siku zinavyozidi kusonga, gharama ya maisha nayo imezidi kupanda hivyo unaweza kujikuta una matumizi makubwa kuliko kipato unachoingiza. imekuwa kawaida kwa watu wengi hususani vijana kufanya harakati nyingine ile mradi tu wapate fedha.

Unataka kutengeneza kipato cha ziada ukiwa nyumbani? Unaweza kufanya hivi kwa njia hizi rahisi

Andika CV: Kuna soko kubwa katika ajira hii kwani idadi ya watu wanaotafuta kazi ni kubwa. Kama wewe ni mwandishi mzuri unaweza kufanya kazi hii ambayo uendeshaji wake unahitaji gharama ndogo tu. Unaweza kutangaza huduma zako kupitia mitandao kama LinkedIn ili kuwafikia watu wengi zaidi na kutengeneza kipato kikubwa. Aina hii ya ajira ni nzuri kwani itakuwezesha kutekeleza majukumu yao mengine bila muingiliano wowote.

FUNDISHA KUPITIA SKYPE: Unaweza kuwa mwalimu na kutoa mafunzo kwa watu kutoka maeneo mbalimbali kupitia teknolojia ya video ya Skype. Hakuna haja ya kuwafuata wanafunzi wako hivyo gharama za uendeshaji hi rahisi. Unaweza kutoa mafunzo kwa gharama nafuu na kutengeneza kipato kizuri tu kwa njia hii. Unaweza kutumia mitandao kama Facebook, Instagram na Twitter kutangaza huduma zako na kuwavuta wenye uhitaji.

BIASHARA: Baada ya kutafiti na kutambua soko lako, unaweza kuanzisha biashara ndogo ambayo unaweza kufanya nyumbani au kupitia mitandao ya kijamii. Kwa kufanya hivyo, unaokoa gharama kubwa ya kupangisha duka na kulipa kodi hivyo kuokoa fedha nyingi. Kutokana na mazingira yako, unaweza kuuza bidhaa ambayo uhitaji wake ni ukubwa na kutengeneza faida nzuri. Kwa mfano: unaweza kuuza sabuni kama eneo ulipo kuna uhitaji wa bidhaa hiyo ya maduka yapo mbali au unaweza kuanzisha biashara ndogo ya kuuza juisi kama unaishi karibu na maeneo ya shule.

AIR BNB: Kama una chumba cha ziada nyumbani kwako, kuna soko kubwa la Air BnB. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha chumba au nyumba hiyo ipo katika kiwango kizuri na kisha kuitangaza kwani watu wengi siku hizi wamekuwa wakitumia huduma hii badala ya kwenda hotelini kama ilivyokuwa awali. Unaweza kutengeneza kipato zaidi kwa kutoa huduma za ziada kwa wageni wako kama usafi.

Siku hizi sio lazima uwe na ajira maalum ili kutengeneza kipato kizuri. Katika ulimwengu huu wa teknolojia, unaweza kuwa mbunifu na kujiajiri mwenyewe hata ukiwa nyumbani kwako. Hii ni fursa nzuri kwa wale ambao wanapoteza muda mwingi kutafuta kazi mara tu wanapomaliza elimu yao. Wakati unafanya hivyo, unaweza kuwa mbunifu na kujiajiri mwenyewe kwa mtaji mdogo tu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter