Poland imeahidi kuisadia Tanzania kuimarisha mifumo ya kodi kwa njia ya kidigitali ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa ajili ya kuendeleza nchi na watu wake kwa ujumla.
Ahadi hiyo imetolewa Mjini Davos nchini Uswisi na Waziri wa Fedha wa nchi hiyo Magdalena Rzeczkowsk, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba.
Amesema kuwa mpango huo utatekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo Poland itatumia uzoefu wake katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa njia ya kielektroniki kuifanya Tanzania pia iwe na uwezo huo ili kuimarisha ukusanyaji wa mapato yake ya ndani kwa njia ya kodi.