Home FEDHA TANESCO yaelemewa na madeni

TANESCO yaelemewa na madeni

0 comment 170 views

Malimbikizo ya madeni ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kutokana na kufua umeme kwa kutumia vyanzo ghali miaka ya nyuma imepelekea shirika hilo kuiomba serikali kulipa deni la Sh. 1.39 trilioni wanazodaiwa na taasisi mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Dk. Tito Mwinuka ameeleza kuwa shirika hilo linadaiwa takribani Sh. 950 bilioni na watoa huduma mbalimbali wakiwemo IPTL, Songas, Pan African, TPDC pamoja na Sh. 442 bilioni ambazo walikopeshwa na benki kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Dk. Mwinuka amefafanua kuwa imewabidi kuiomba serikali kuyalipa madeni hayo kwa sababu riba inaendelea kuongezeka kadri wanavyochelewesha malipo, jambo ambalo linadhoofisha shughuli za shirika hilo.

“Tunaiomba serikali kupitia hazina kuyalipa madeni hayo ili kuipunguzia mzigo TANESCO”. Amesema Mkurugenzi huyo.

Aidha, amesema kuwa mabadiliko ambayo wamefanya yanaelekea kuzaa matunda kwani hapo awali walikuwa wakipata hasara kutokana na matumizi ya mafuta mazito ambayo ni ghali. Dk. Mwinuka ameeleza kwa wanatarajia kupata faida mwaka huu kutokana na matumizi nafuu ya gesi.

Mwaka 2016/17, shirika hilo lilipata hasara ya Sh. 265 bilioni. Vilevile mwaka 2017/18 walipata hasara ya takribani Sh. 124 bilioni. Dk. Mwinuka ameeleza kuwa kufuatia mabadiliko kwenye ufuaji umeme, mwaka huu wanatarajia kupata faida ya Sh. 9 bilioni.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter