Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesema imekusanya Tsh trilioni 5.923 sawa na ufanisi wa 99.1% ya lengo katika kipindi cha robo ya mkwanza ya wamaka wa fedha 2022/23.
Lengo la TRA ilikuwa ni kukusanya Tsh trilioni 5.978 kwa kipindi hicho cha Julai hadi Septemba.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata, makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la 14.6% ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha uliopita.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, kwa mwezi Setemba 2022, TRA imekusanya Tsh trilioni 2.273 ikilinganishwa na lengo la kukusanya Tsh trilioni 2.154.
“Makusanyo haya ni sawa na ufanisi wa 105.5% na ukuaji wa 14.3% ikilinganishwa na mwezi Septemba 2021 ambapo makusanyo yalikuwa trilioni 1.989,” amesema Kidata.