Home FEDHA Ukuta waongeza mapato Mererani

Ukuta waongeza mapato Mererani

0 comment 119 views

Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini, Prof. Shukrani Manya amesema kuanzia mwezi Aprili hadi Desemba mwaka jana, serikali imefanikiwa kukusanya takribani Sh. 1.43 bilioni kwenye madini aina ya Tanzanite pekee, kutokana na ujenzi wa ukuta kwenye machimbo ya madini hayo eneo la Mirerani.

Prof. Manya ameeleza hayo alipokuwa kwenye mafunzo ya madini kwa waandishi wa habari na kuongeza kuwa, lengo kuu la ukuta huo ambao umegharimu Sh. 6 bilioni ni kuzuia kukwepa kodi pamoja na wizi wa madini. Aidha, Prof. Manya amesema fedha hizo zilizopatikana zimetokana na makusanyo ya kilogramu 781.2 za madini hayo ambapo kwa mwaka 2016 zilikusanywa kilo 164.6 ambazo zilizalisha Sh. 71.8 milioni na mwaka 2017 zilipatikana Sh. 166 .1 kutoka kwenye kilo 164.6 walizokusanya.

“Kwa hiyo ujenzi wa ukuta umesaidia kuongeza mapato na kudhibiti madini yaliyokuwa yakipotea, haya ni mafanikio na mwaka huu 2019 tunatarajia kuongeza mapato zaidi”. Amesema Mtendaji huyo.

Akizungumzia masoko ya madini yanayoendelea kufunguliwa sehemu mbalimbali hapa nchini, Prof. Manya amesema uwepo wa masoko hayo utasaidia upatikanaji wa takwimu sahihi na kuweka kazi kuwa changamoto iliyopo hivi sasa ni uchache wa watumishi.

“Tangu Machi 27 mwaka huu tulipofungua soko la Geita, tayari kilo 167 za madini zimepitishwa sokoni”. Amesema.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter