Home FEDHA Wadaiwa kodi ya ardhi kusakwa nyumba kwa nyumba

Wadaiwa kodi ya ardhi kusakwa nyumba kwa nyumba

0 comment 99 views

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametangaza kampeni maalum ya nyumba hadi nyumba inayolenga kuwasaka wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi ambao hawajalipa madeni yao hadi kufikia mwaka huu. Lukuvi amezindua kampeni hiyo wilayani Karatu mkoani Arusha wakati akisikiliza na kutatua migogoro ya ardhi ya wakazi wa wilaya hiyo katika kampeni ya Funguka kwa Waziri na kuwataka watendaji wote wa wilaya na kanda nchini kupita nyumba kwa nyumba kuwatafuta wadaiwa wa kodi ya ardhi.

“Naagiza mikoa yote ya Tanzania Bara kuanza kampeni rasmi ya kuwasaka wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi ya nyumba kwa nyumba na msiwaonee huruma hata kama ni Waziri na anadaiwa kodi ya ardhi peleka mahakamani hata kama ni kiongozi yeyote, hata kama Mkuu wa Wilaya mfuate na peleka mahakamani”. Amesema Lukuvi.

Waziri huyo ametoa wito kwa wanaomiliki ardhi kujitathmini na kukagua taarifa zao huku akiwataka wale ambao hawajalipa kufanya hivyo mara moja kabla kampeni haijawafikia. Amewataka watendaji kutokuwa na huruma na wadaiwa kwani fedha za kodi hutumika katika ujenzi wa miundombinu na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter