Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Mara X na Z ‘smartphone’ za kwanza kuzalishwa Afrika

Mara X na Z ‘smartphone’ za kwanza kuzalishwa Afrika

0 comment 99 views

Imekuwa ni kawaida kuona kampuni mbalimbali za teknolojia zinaagiza  vifaa mbalimbali vya simu kutoka mabara mengine na kuja kufanya ‘Assembling’ barani Afrika. Lakini Mara Group, kampuni ya teknolojia iliyopo Rwanda imekuwa ni kampuni ya kwanza kuzalisha yaani kufanya ‘Manufacturing’ simu janja barani humu. Kampuni hiyo ilitengeneza historia mwezi huu kwa kuzindua rasmi simu mbili ambazo ni Mara X na Mara Z.

Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni hiyo, Ashish Thakkar, ameeleza kuwa kampuni hiyo ina uwezo wa kuzalisha simu hizo 1,200 kwa siku na wana mpango wa kuzalisha hadi simu milioni 2 kila mwaka. Licha ya kuwa simu hizo zinauzwa bei kubwa kidogo ikilinganishwa na washindani kama Tecno (kampuni ya wachina) , Kampuni hiyo inategemea waafrika hasa Warwanda  kununua simu hizo ili kuweza kuhamasisha uzalishaji zaidi wa bidhaa hiyo. Pia kampuni hiyo ina mpango wa kufanya majadiliano na benki mbalimbali ili kuweza kuwarahisishia wateja wa simu hizo kufanya manunuzi kwa urahisi ikiwa ni pamoja na kuchukua simu hizo huku wakiendelea kulipia simu hizo taratibu ndani ya miaka miwili.

Simu ya Mara X ina sifa zifuatazo: katika upande wa Display simu hiyo ina inchi 5.5-inch HD+ (720×1440), Prosesa ya MediaTek MT6739 SoC, RAM ya GB 1, na sehemu ya kuhifadhia kumbukumbu yenye uwezo wa 16GB. Kamera ya nyuma ina 13MP na sense ya fingerprint huku kamera ya mbele ikiwa na 5MP.

Na kwa upande wa simu ya Mara Z, simu hiyo ina sifa zifuatazo: simu hiyo ina Display ya inchi 5.7 HD+, Prosesa ya Qualcomm Snapdragon 435, RAM ya GB 2, na sehemu ya kuhifadhia kumbukumbu ina uwezo wa GB32. Pia katika upande wa kamera simu hiyo ina kamera yenye uwezo wa 13MP na sensa ya fingerprint kwa nyuma, na kamera ya mbele pia ina 13MP. Aidha simu hiyo ina mfumo wa Android wa 8.1 Oreo.

Licha ya kuwa kampuni hiyo inatengeneza vifaa karibia vyote vinavyotumika kutengeneza simu hizo, lakini imeelezwa kuwa kampuni hiyo bado inalazimika kuagiza nje ya nchi baadhi ya vifaa kwamfano Prosesa zilizotumika kutengeneza simu hizo.

Aidha, katika upande wa bei simu ya Mara X inauzwa Franc 175,750( takribani dola  190 ambayo ni sawa na shilingi 436,278.95 kwa Tanzania) huku simu ya Mara Z ikiuzwa Franc 120,250 (takribani dola 130 ambazo ni sawa na shilingi 298,506.65 kwa Tanzania).

Je, una maoni gani kuhusu simu hizi? tuandikie maoni yako

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter