Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Museveni asema EAC watanufaika na mradi wa mafuta

Museveni asema EAC watanufaika na mradi wa mafuta

0 comment 111 views
Na Mwandishi wetu

Rais Yoweri Museveni wa nchini Uganda amesema ni wakati wa nchi za Afrika Mashariki kukua na kuendelea kiuchumi kwani nchi za ukanda huu zimebarikiwa kila kitu hivyo hakuna sababu ya kutopiga kasi katika maendeleo.

Kuhusu mradi wa bomba la mafuta, Rais Museveni amesema kuwa, japo kuwa mradi huo unahusisha nchi za Tanzania na Uganda pekee, manufaa yake yatakuwa kwa nchi zote za Afrika Mashariki kwani kuna njia nyungi za kunufaika mbali na usafirishaji wa mafuta pekee.

Ameongeza kuwa manufaa ya mradi huu ni kwa nchi zote za Afrika Mashariki hivyo wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)wanapaswa kuangalia mradi huu kama mali ya jumuiya yote. Pia Rais Museveni ameshauri nchi za Afrika Mashariki pamoja na Afrika kwa ujumla kuachana na utamaduni wa kuzalisha vitu tusivyovitumia na kutumia vitu tusivyovizalisha kwani tamaduni hii inarudisha nyuma maendeleo.

Ujenzi huu wa bomba la mafuta unafanywa na kampuni za Total E&P,CNOOC na Tullow Oil kuwa ushirikiano na serikali za Uganda na Tanzania. Bomba hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1,445 huku kilometa 1,149 zikiwa katika mikoa nane ya Tanzania na kilometa 296 zikiwa nchini Uganda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter