Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Tanzania kuisaidia Sudan Kusini kuimarisha mapato

Tanzania kuisaidia Sudan Kusini kuimarisha mapato

0 comment 78 views

Tanzania inatarajia kuingia makubaliano na Sudan Kusini kuisaidia kuimarisha Mamlaka ya Mapato nchini humo.

Serikali itaingia makubaliano hayo kupitia Chuo cha Kodi Tanzania (ITA) kutokana na mafunzo yatolewayo chuoni hapo ya masuala ya ushuru, kodi na forodha.

Mkuu wa chuo hicho Prof. Isaya Jairo alisema “Afrika Mashariki iliteuwa chuo hiki kuwa kituo cha umahiri katika mafunzo kuhusu masuala ya kodi, ushuru na forodha. Tunaendelea na mazungumzo na Sudan Kusini tunawasaidia kuimarisha mamlaka ya mapato”.

Prof. Jairo alikuwa akizungumza kuhusu mahafali ya 13 ya chuo hicho ambapo takribani wahitimu 389 wanatarajiwa kutunikiwa vyeti katika ngazi ya shahada, stashahada na astashahada.

Katika mahafali hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. Pia yatahudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo makamishna wa kodi kutoka Sudani Kusini na Comoro.

Alieleza kuwa ITA imepeleka maombi ya mtaala mpya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ili kuwa na mafunzo yanayoendana na mabadiliko ya sayansi, teknolojia na uchumi.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter