Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Tanzania, Msumbiji kujadili biashara, uwekezaji

Tanzania, Msumbiji kujadili biashara, uwekezaji

0 comment 97 views

Tanzania na Msumbiji wanatarajiwa kushiriki mazungumzo ya pamoja ambayo yatajikita katika sekta ya biashara, uwekezaji, ulinzi na usalama.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika Julai 02, 2024 ambapo Rais wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi atafanya ziara ya Kiserikali ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia na Rais Nyusi, watashuhudia utiaji saini wa makubaliano katika sekta mbalimbali za ushirikiano.

Taarifa kutoka Ikulu inasema ziara “ziara hii itaendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria, kidugu na kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji ambao uliasisiwa na viongozi wetu, kiongozi wa kwanza wa chama cha nchi hiyo (FRELIMO), Hayati Eduardo Chivambo Mondlane na Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere.”

Aidha, Rais Nyusi anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) Julai 03, 2024 ambapo ataambatana na mweneyeji wake Rais Samia.

Rais huyo wa Msumbiji anatarajiwa kuondoka nchini Julai 04, 2024.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter