Jiajiri mtandaoni leo

0 comment 113 views

Mtandao ni moja kati ya uwekezaji ambao hakuna haja ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye majengo au kupanga kwa ajili ya ofisi. Matumizi ya mitandao yameendelea kuwa soko linalozidi kukua kwa mtu yeyote anayefikiria kuanzisha biashara ya mtandaoni.

Kama wewe unafikiria kumiliki biashara mtandaoni, mawazo yafuatayo yanaweza kukupa muelekeo utakaokuwezesha kufikia malengo yako.

Kuanzisha blogu

Kama wewe ni mwandishi unaweza kuanzisha blogu yako na kuandika makala au habari mbalimbali. Unachotakiwa kuzingatia ni mahitaji ya walengwa wako na kuwapa kile wanachotaka. Kama wewe ni shabiki mkubwa wa masuala ya mpira basi blugu yako ihusiane na michezo. Kupitia blogu, unaweza kujiingizia kipanto kutokana na matangazo na idadi ya watu wanaopitia habari zako.

Kuwa meneja wa mitandao ya kijamii

Biashara nyingi hivi sasa zimejikita kwenye mitandao ya kijamiii ili kuwafikia watu wengi kwa urahisi zaidi. Ikiwa una ujuzi wa kutosha wa mitandao kama Facebook na Instagram, unaweza kutumia fursa hiyo kuingiza kipato kwa kusimamia mitandao ya biashara na kutangaza kampuni au taasisi huzika.

Kutoa mafunzo

Badala ya kutumia muda mwingi kutafuta ajira, unaweza kutumia nafasi hiyo kutoa mafunzo ya kitu ambacho una uelewa na ujuzi nacho kupitia mitandao mbalimbali. Kwa mfano, kama wewe ni mpishi mzuri, unaweza kufungua chaneli ambayo itatoa mafunzo kuhusu mambo ya mapishi. Unaweza kufundisha kuhusu ujasiriamali, urembo, hisa n.k.

Kutoa huduma za SEO

Sekta ya SEO imeendelea kukua kwa kasi duniani kote. Kama wewe ni mtaalamu unaweza kutoa huduma hii kwa makampuni na vyombo vya habari na kujitengenezea kipato.

Kufungua chaneli Youtube

Katika ulimwengu huu wa digitali, mtandao kama Youtube hutembelewa na maelfy ya watu kila siku. Unaweza kutumia fursa hiyo kuanzisha chaneli yako na kuweka video. Utakapopata wafuasi wa kutosha, unaweza kuingiza fedha kwa kutumia Google Adsense ambayo hutumika kuweka matangazo kwenye video.

Kuanzisha Podcast

Podcasting ni njia nyingine nzuri kwa wajasiriamali kupata fedha. Unaweza kuanzisha podcast yako mwenyewe na kuuza matangazo ya ‘ad’ au pamoja na wafadhili walio karibu na maudhui yako.

Kuuza bidhaa eBay au Etsy

Kama una bidhaa unazotaka kuweka sokoni, anzisha duka la mtandaoni kwenye majukwaa kama eBay ili kuuza bidhaa zako. Kama wewe ni mtaalamu wa kutengeneza bidhaa za mkono, mtandao wa Etsy ni sehemu mahsusi kwa ajili ya kuuza vifaa hivyo. Unaweza kuanzisha duka lako hapo na kufanya biashara.

Uhariri

Watu binafsi, wafanyabiashara pamoja na vyombo mbalimbali vya habari wana uhitaji mkubwa wa wahariri. Ikiwa wewe ni mtu makini kwenye masuala haya, unaweza kufanya kazi hii mtandaoni na kuingiza kipato kizuri.

Kuanzisha mtandao wa matangazo

Unaweza kuanzisha mtandao maalum ambao unalenga kutangaza biashara binafsi pamoja na zile za mashirika za mtandaoni na kutengeneza fedha kupitia matangazo hayo.

Mshauri wa masuala ya usafiri

Watu hupenda kusafiri na mara nyingi wanatafuta mawakala watakaowasaidia kwa mikataba bora. Hivyo basi, unaweza kuwa mshauri wa kusafiri mtandaoni ili kuwasaidia wateja kupata mikataba ya chaguo la kusafiri na kupendekeza vifurushi bora.

Kuna fursa kemkem za kufanya biashara mitandaoni. Kinachotakiwa ni kupata wazo zuri, kulitumia ipasavyo kijiingizia kipato na kufanya kazi kwa bidii.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter