Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI JINSI VIJANA WALIVYO NA NAFASI NZURI KATIKA NJIA YA MAFANIKIO

JINSI VIJANA WALIVYO NA NAFASI NZURI KATIKA NJIA YA MAFANIKIO

0 comment 182 views

Kila kijana ana ndoto za kufanikiwa kimaisha,kutokana na umri wao kuwaruhusu kufanya mabadiliko chanya katika maisha yao na kua njia sahihi ya kuleta mabadiliko katika jamii nzima,baadhi ni sababu zinazoweza kufanya wepesi katika kupata mafanikio

  • Uthubutu wao wa kujaribu vitu tofauti

Tofauti na makundi mengine, vijana wamekuwa mstari wa mbele kujaribu biashara au shughuli mbalimbali na hivyo kufahamu soko katika taswira zaidi ya moja. Kufanya hivi kumesaidia vijana wengi kujua ni nini hasa aina mbalimbali ya wateja wanataka hivyo kuwaweka katika nafasi nzuri zaidi ya kufanya biashara ambayo itaendana na mahitaji ya jamii inayowazunguka kwa wakati huo.

  • Vijana wamekuwa wabunifu na wanaendana na wakati

Kipindi cha huko nyuma, waliojikita katika ujasiriamali walikuwa wanafanya tu shughuli zao pasipo kuzingatia ubunifu na utofauti ili kujiweka katika nafasi ya juu kwa wateja wao. Hali kwa sasa ni tofauti, vijana ambao kadri siku zinavyokwenda ndio wamekuwa wakijikita zaidi katika ujasiriamali wamekuwa sio tu wafanyabiashara bali wabunifu katika kile wananchofanya na idadi kubwa wameonyesha kufanikiwa kutokana na kujitofautisha na wengine.

ADVERTISEMENT

  • Wapo katika nafasi nzuri zaidi ya kufanya utafiti na kuepuka kufanya makosa yaliyofanywa na wengine

Vijana wengi wameweka nia ya kujifunza, kufanya utafiti na kufahamu soko vizuri kabla ya kuwekeza katika biashara au shughuli fulani kwa asilimia zote. Wengi wamekuwa wakijifunza kutoka kwa wajasiriamali wengine ambao wamekuwepo kwa muda mrefu, kupitia matamasha pamoja na makongamano ambayo hutangazwa na mashirika au taasisi na wadau mbalimbali wa maendeleo. Kufanya hivyo kumesaidia wengi wao kuepuka makosa ambayo pengine hufanywa na watu wengi, hali ambayo imewaweka katika nafasi nzuri ya kufanikiwa.

  • Mitandao ya kijamii

Katika karne hii ya teknolojia, mitandao ya kijamii ina nchango mkubwa sana katika biashara, ujasiriamali na ukuaji wa uchumi. Kwa vijana, hii imekuwa njia rahisi zaidi ya kuzungumza, kushauriana na kutangaza kile unachofanya. Mitandao kama Instagram na Facebook imekuwa na matokeo mazuri kibiashara kwani imesaidia kufikisha huduma maeneo mbalimbali mnchini kirahisi. Vijana wengi wamekuwa wakitumia fursa hii kukuza na kuimarisha biashara zao.

  • Mipango na Majukumu

Enzi za wazazi wetu, wajasiriamali wengi tayari walikuwa na majukumu au mipango mengine hivyo walishindwa kuwekeza muda wao wote katika biashara. Wengi tayari walikuwa wazazi, walezi au wakifanya vitu vingine ambavyo vilipelekea majukumu kama biashara kutokuwa kipaumbele. Hivi sasa, vijana wengi kabla hata ya kuwekeza rasmi katika ujasiriamali hujiwekea mipango na mikakati madhubuti hivyo kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kuhakikisha malengo waliyojiwekea yanatimia.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter