Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Vitambulisho vya Magufuli vyaanza kutolewa Tabora

Vitambulisho vya Magufuli vyaanza kutolewa Tabora

0 comment 51 views

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewaonya wajasiriamali wadogo mkoani humo kutotumia vitambulisho vilivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kufanya biashara za wafanyabiashara wakubwa kwani vitendo hivyo ni ukwepeji kodi. Mwanri amesema hayo wakati akigawa vitambulisho 25,000 kwa wakuu wa wilaya saba za mkoa huo na viongozi watatu wa wajasiriamali kutoka manispaa ya Tabora kuashiria uzinduzi wa zoezi hilo mkoani humo. Mkoa huo ulipatiwa jumla ya vitambulisho 25,000 na halmashauri zote nane za Tabora zimepata vitambulisho 3,125.

Mkuu huyo amesema vitambulisho vilivyotolewa na Rais ni maalum kwa wajasiriamali wadogo na sio vinginevyo. Ni kwa ajili ya kundi la watu ambao biashara zao kwa siku zote 365 za mwaka hazizidi mapato ya Sh. 4 milioni. Mwanri ameongeza kuwa kwa mujibu wa Sheria ni kosa kuazimisha kitambulisho au kubeba bidhaa za wafanyabiashara wakubwa na kusisitiza atakayebainika atafikishwa katika vyombo vya Sheria na hatua zaidi zitachukuliwa.

Naye Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani humo Thomas Masese amesema wanaostahili kupata kitambulisho hicho ni walio na mauzo ghafi yasiyozidi Milioni 4 kwa mwaka. Ameeleza kuwa wafanyabiashara hao watatakiwa kulipia Sh. 20,000 kwa ajili ya kitambulisho baada ya kujaza fomu maalum inayopatikana kwa Mkuu wa mkoa au wilaya.

Aidha Meneja huyo ametangaza kuwa kuanzia sasa, vitambulisho vilivyokuwa vikitolewa na mamlaka hiyo kwa ajili ya wajasiriamali vimesitisha na vitakavyotumika sasa ni vile ambavyo vimetolewa na Rais Magufuli.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter