Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI SIDO yatoa mafunzo ya ubanguaji korosho kwa wajasiriamali Lindi

SIDO yatoa mafunzo ya ubanguaji korosho kwa wajasiriamali Lindi

0 comment 109 views

Ofisa Uendelezaji Mafunzo kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) Isack Daniel amesema Shirika hilo limewapatia mafunzo ya ubanguaji korosho kwa  wajasiriamali 48 kutoka wilaya za Lindi na Nachingwea mkoani Lindi. Katika mafunzo hayo, wajasiriamali wamejifunza hatua za ubanguaji bora wa korosho, teknolojia, usalama na afya kiwandani. Ofisa huyo ameeleza kuwa, mafunzo hayo yanalenga kuongeza kasi ya uongezaji wa thamani katika zao la korosho ili wananchi waweze kupata ajira na kutengeneza kipato kupitia ubanguaji.

Mbali na hayo, mambo mengine waliyojifunza wajasiriamali hao ni ubora, usalama na usafi wa chakula (korosho) katika uzalishaji, matumizi na matengenezo madogo madogo katika mashine za ubanguaji, upangaji wa madaraja, ufungashaji na utunzaji wa madaraja kwa korosho ambazo tayari zimebanguliwa.

Kwa upande wake Meneja wa SIDO mkoani Lindi, Mwita Kasisi amesema mafunzo hayo ni endelevu katika wilaya nyingine na yatafanyika kulingana na mahitaji ya wilaya husika.

“Baada ya mafunzo hayo washiriki wataweza kupata ajira kutokana na viwanda vya ubanguaji wa korosho vitakavyofunguliwa na wengine watakwenda kuanzisha viwanda vyao ambavyo vitatengeneza ajira kwa wananchi wengine”. Ameeleza Kasisi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter