Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Sifa 5 za mjasiriamali bora

Sifa 5 za mjasiriamali bora

0 comment 175 views

Kila mtu ana ndoto ya kumiliki biashara au mradi wake mwenyewe na kuwa mjasiriamali lakini jambo hili sio rahisi kama wengi tunavyofikiria. Mjasiriamali anatakiwa kuwa sifa fulani ili aweze kufikia malengo yake na kufanikiwa katika safari yake ya ujasiriamali.

Hizi hapa ni sifa tano za mjasiriamali bora

Ujasiri

Hii ni moja kati ya sifa muhimu zaidi kwa mjasirimali kwani ujasiri ni nguzo ya mafanikio. Ujasiriamali unahitaji ujasiri mkubwa wa kuchukua maamuzi magumu pale ambapo mambo hayaendi kama ulivyopanga. Ikiwa huna ujasiri wa kutosha, ni vigumu sana kuwekeza fedha na muda katika biashara yako.

Malengo

Malengo yatakuwezesha kufanikisha jambo lolote. Kuwa na malengo ni sifa muhimu ambayo kila mjasiriamali anapaswa kuwa nayo. Malengo yatakuongoza ufanye nini, wapi, lini na kwa ajili ya nini. Bila malengo utafanya mambo bila kuwa na muongozo maalum na itakuwa ngumu zaidi kufanikiwa.

Ubunifu

Ubunifu ni kitu pekee kinachomtofautisha mjasiriamali mmoja na mwingine. Unahitaji kuwa mbunifu ili kuja na wazo la pekee ambalo litakupa matokeo mazuri na kutimiza malengo uliyonayo. Wajasiriamali wengi wanakwama kwa sababu wanakosa ubunifu hivyo wanaishia kufanya kitu ambacho kila mtu tayari anafanya hivyo kushindwa kujitofautisha sokoni.

Kuishi vizuri na watu

Kila mjasiriamali anahitaji watu wengine ili kufanikisha malengo yake. Kuishi na watu vizuri ni sifa muhimu kwani inamjengea mjasiriamali soko na nguvu kazi bora. Kama mjasiiamali, hakuna haja ya kudharau watu wanaokuzunguka bila sababu za msingi. Usijenge chuki kati yako na watu wengine kwani watu hao ndio chanzo cha mafanikio.

Kujifunza

Makosa ni shule muhimu kwa kila mtu, ndivyo ilivyo pia kwa mjasiriamali. Kila mjasiriamali anatakiwa kupenda kujifunza kutokana na makosa ili aweze kuyaepuka mbeleni. Changamoto zipo kila mahali hivyo unapokosea, kuwa na moyo wa kujifunza na sio kukata tamaa. Jifunze kutokana na makosa, kupitia wateja wakp na vilevile kutoka kwa wajasiriamali wengine.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter