Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Unafanya urembo wa nywele? Soma hii

Unafanya urembo wa nywele? Soma hii

0 comment 153 views

Kila mtu hupendelea kuwa na sehemu maalum kwa ajili ya kutengeneza nywele zake, kwa sababu sio kila mahali panaweza kutimiza matakwa ya kila mtu na ndio maana utakuta mteja anatengeneza nywele zake sehemu moja kwa miaka hata zaidi ya kumi kutokana na kuridhishwa na huduma inayotolewa. Kama unafanya kazi katika saluni basi ni muhimu kutekeleza majukumu yako na kuhakikisha unatimiza matakwa ya mmiliki na mteja, pia ikiwa unamiliki saluni basi ni muhimu kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

Hapo chini ni baadhi ya vitu ambavyo biashara ya aina hii inapaswa kuzingatia ili kufikia malengo yake.

Usafi- Muonekano wako, saluni yako, na wafanyakazi wako humpa picha kamili mteja pindi tu anapowasili. Hivyo ni muhimu kuwa nadhifu, kuweka mazingira safi na salama, na kuhakikisha wafanyakazi wote wanafanya kazi katika hali ya usafi. Pia

Ukarimu na kujifunza kutoka kwa wateja- Ni vyema kujua kila mteja atakuwa ni tofauti hivyo jifunze kuwa mkarimu kwa wateja wote bila kubagua. Kwa kufanya hivyo itakurahisishia kutengeneza wateja waaminifu, itakusaidia kupata wateja zaidi kwa sababu mteja mmoja akifurahishwa na huduma yako ni rahisi kwa mteja huyo kuwaleta watu wengine. Pia kwa kupitia wateja utajifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na namna ya kufanya kazi yako vizuri zaidi.

Nenda na wakati- Unajua kinachoendelea ulimwenguni? Ulitazama habari jana usiku? Kuweka mazungumzo ya kisasa inasaidia na inaonyesha kuwa upo tayari kujifunza. Nenda na wakati sio tu kwa mambo yanayoendelea dunaini bali kwenda na wakati hata kuhusu masuala yanayohusiana na tasnia yako kwani mitindo inabadilika kila siku. Hakikisha hupitwi na mabadiliko hayo.

Malengo- Wakati unafungua biashara yako ni dhahiri kuwa ulikuwa una malengo ambayo mwisho wa siku unataka kutimiza. Inashauriwa kutenganisha malengo katika sehemu mbili: malengo ya muda mfupi na ya muda mrefu. Hakikisha unapitia malengo yako kwa ujumla ili kuona kama unakwenda katika njia sahihi na vitu gani ufanye ili kuweza kuyafikia. Kwa mfano weka muda wa kutosha kwa ajili ya kufanya tathmini ili kujua wapi unatakiwa kuboresha na vitu gani vya kuacha.

Kila biashara huja na changamoto zake lakini ili kuweza kufanikiwa, siku zote epuka kufanya maamuzi kutokana na hisia kwa kufanya hivyo unaweza kujikuta unapoteza wafanyakazi, wateja, na watu wengine wanaochangia katika biashara yako. Kabla hujafanya maamuzi tafakari kwa makini, omba ushauri kwa watu wengine wenye uzoefu zaidi yako ili kuhakikisha biashara yako haiathiriwi na maamuzi mabaya.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter