Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Antony Mavunde amesema Programu ya Feed the Future inayofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) inatarajia kuwanufaisha vijana 30,000 kutoka Iringa, Mbeya na mikoa mingine ya Tanzania visiwani. Mavunde amesema hayo alipokuwa akizindua Baraza la Vijana la Ushauri wa Miradi na kuongeza kuwa, kupitia fursa ya kilimo na ujasiriamali, vijana watapewa nyenzo na mitaji yenye thamani ya Sh. 11 bilioni ili kuanza hatua ya uzalishaji.
Soma Pia Vijana kutengewa maeneo ya uzalishaji.
Akizungumzia ufadhili huo, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dr. Imni Patterson amesema serikali ya Marekani itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuwapa vijana ujuzi na uwezo wa uzalishaji mali katika sekta ya kilimo kutokana na sekta hiyo kutoa ajira kwa watanzania wengi ukilinganisha na sekta nyinginezo.
Soma Pia Mhagama ahamasisha vijana kuwekeza shambani
Kwa Upande wake Kaimu Mkuu Mkoa wa Iringa, Richard Kasesela ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa baraza hilo ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kama ulivyopangwa ili kuwanufaisha vijana walio wengi mkoani humo.