Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Vijana washauriwa kuanzisha miradi kimkakati

Vijana washauriwa kuanzisha miradi kimkakati

0 comment 106 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama ametoa wito kwa vijana kubadilisha mtazamo kwa kuwa wabunifu na kuanzisha miradi ya kimkakati itakayowawezesha kiuchumi. Mhagama amesema hayo mkoani Iringa wakati akihamasisha na kukagua maeneo ya ujenzi wa vitalu nyumba (Green House) na uwepo wa miundombinu itakayotumika kwenye maeneo hayo.

Waziri Mhagama ameeleza kuwa sekta ya kilimo inaajiri na kuchangia zaidi ya asilimia 60 katika pato la taifa hivyo vijana ambao ndio nguvukazi ya taifa wanapaswa kuitumia rasilimali ardhi kama mtaji wa kujiajiri na kuajiri wengine.

“Lengo letu ni vijana kutumia sekta hii ya umahiri kwa ajili ya kuwaondoa kwenye mitazamo finyu na kuwa na mitazamo chanya ili waweze kunufaika na miradi itakayobuniwa na kutumika kama mfano kwa vijana nchi nzima”. Amesisitiza Mhagama.

Aidha Waziri huyo amesema kuwa vijana watapatiwa elimu ya kilimo cha kitalu nyumba ambayo itawapa nafasi ya kuongeza thamani kwenye mazao watakayozalisha na mradi huo kuwa sehemu ya ajira zao. Vilevile, Mhagama amewashauri vijana kushirikiana na kuwa chachu ya maendeleo ya uchumi wa taifa kwa kushirikiana kwa pamoja ili kutimiza azma ya vijana wote bila kujali itikadi wala tofauti zao.

Naye Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amesema mradi huo utawawezesha vijana kuondokana na ugumu wa ajira kwani serikali imewaletea teknolojia hiyo itakayowawezesha kujiajiri.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter