Home BIASHARA Huduma za kifedha kupitia simu za mkononi zinachochea kukua kwa mfumo rasmi wa kifedha nchini Tanzania

Huduma za kifedha kupitia simu za mkononi zinachochea kukua kwa mfumo rasmi wa kifedha nchini Tanzania

0 comment 108 views

Kuimarika kwa mfumo rasmi wa kifedha ni moja ya nguzo katika maendeleo ya jamii yoyote au nchi, na suala hili limeweza kufanyika nchini Tanzania.Labda kwanza tufahamu maana ya neno mfumo rasmi wa fedha? Kulingana na Benki ya Dunia, kuingizwa katika mfumo rasmi wa kifedha, ina maana kwamba watu na wafanyabiashara wanapata huduma  za kifedha zinazofaa na za gharama nafuu  kulingana na matakwa yao, mfano wa huduma hizo ni kama vile kufanya mihamala ya malipo mbalimbali,kuweka akiba,kupata mikopo na huduma za bima.Huduma hizi kwa kipindi kirefu nyuma wamekuwa wakizipata watu wenye akaunti za benki ambazo ziko katika majina yao binafsi zinazoonyesha pia jina la taasisi ya fedha ambazo wanazo akaunti zao.

Mfumo rasmi wa kifedha hupimwa kutokana na asilimia ya watu wazima (waliofikisha umri wa miaka 15), ambao angalau wana akaunti moja kwa majina yao binafsi katika taasisi inayotoa huduma za kifedha ambayo inaendeshwa kwa kufuata kanuni za usimamizi za serikali.

Mfumo huu huwezesha wenye akaunti binafsi kwenye taasisi za kifedha kuweza kupata huduma mbalimbali za kifedha ikiwemo-kujiwekea akiba, kupata mkopo, kutuma fedha, huduma za bima na uwekezaji. Taasisi za kifedha zinazotamblika kutoa huduma za kifedha nchini ni pamoja na mabenki, watoa huduma za fedha kupitia mitandao ya simu kama vile M-PESA ya Vodacom Tanzania, taasisi nyinginezo zilizosajiliwa kutoa huduma hiyo ambazo sio mabenki na vyama vya ushirika.

Mnamo mwaka wa 2017, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Tanzania (BOT) iliona umuhimu wa kuchochea mabadiliko ya wananchi wengi kuingia kwenye mfumo rasmi wa kifedha kupitia utekelezaji wa Mwongozo wa Taifa wa Kuwezesha Wananchi wengi kuwa kwenye mfumo rasmi wa kupata huduma za kifedha wa (NFIF) 2014-2016, ambao ulifanikisha kuboresha sheria za kifedha zilizokuwepo na mpya sambamba na kuanzishwa kwa ushirikiano katika miradi baina ya serikali na sekta binafsi.

Hatua hizi zilisababisha uwekezaji mkubwa mojawapo ikiwa katika sekta ya mawasiliano ambapo makampuni ya simu za mkononi yaliwekeza nchini Tanzania.Uwekezaji huo sasa umefanikisha kwa kiasi kikubwa watu wengi kuingia kwenye mfumo rasmi wa fedha kupitia huduma zinazotolewa kupitia mitandao ya simu za mkononi.

Kwa kusimamia na kuhakikisha sheria zinatekelezwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilichukua hatua nzuri. Kulingana na takwimu, asilimia 74% ya wakazi waliishi ndani ya umbali wa kilometa 5 kufikia sehemu za kupata huduma wanazohitaji mwaka 2017. Pia, 56% ya kundi la watu wazima nchini Tanzania, walikuwa kwenye mfumo rasmi wa fedha kupitia akaunti zao walizokuwa wamefungua kwenye taasisi ya kifedha zilizowawezesha kupata huduma za kifedha kupitia akaunti zao.

Kuwepo kwa idadi ya asilimia kubwa ya wananchi katika mfumo rasmi wa kifedha ulichangiwa na kuanzishwa kwa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi, Asilimia 55% ya watu wazima walikuwa na akaunti za fedha za simu, ambapo asilimia 9% walikuwa na akaunti wenye benki tofauti tofauti za benki. Huduma za kifedha kupitia huduma za simu za mkononi zimekubaliwa na wananchi wengi kutokana na urahisi na upatikanaji wake.

Hata hivyo, kuna suala jingine kwenye safari ya kuingizwa watu wengi zaidi katika mfumo rasmi wa kifedha nchini Tanzania, ambalo linahitajiwa kufanyiwa kazi nalo ni kutozingatia usawa wa kijinsia.Upatikanaji wa huduma za kifedha kwenye taasisi zilizokuwa zinatoa huduma hizo miaka ya nyuma zilitumia sheria ambazo zilikuwa hazitoa nafasi kwa wanawake kupata huduma za kifedha kwa urahisi hasa maeneo ya vijijini.Wanawake walichukuliwa kama watu wa kukaa nyumbani na kutunza familia  na kazi ya kutafuta pesa ilikuwa nu jukumu la wanaume pekee.Majukumu ya kifamilia yaliwafanya wanawake kutopata nafasi ya kwenda kwenye mabenki kutafuta njia za kupata huduma za kifedha.

Mfumo rasmi wa kifedha ambao umekuwepo siku nyingi wa kupata huduma za kifedha kwenye mabenki kihistoria umekuwa ukipendelea Wanaume. Kutokana na majukumu ya wanawake ilikuwa ni vigumu kupata huduma za kibenki, hata ambao wangepata nafasi ya kwenda kwenye mabenki kumekuwepo na vikwazo mbalimbali kwao kama vile kuwa na kitambulisho au nyaraka za udhamini kuweza kupata huduma mbalimbali zitolewazo na mabenki.

Tangu mwaka 2008, ilipoanzishwa  huduma ya M-PESA ya Vodacom, huduma za  kifedha kupitia simu ya mkononi  zimeongezeka kwa kasi na kiasi kikubwa nchini hadi kufikia hatua ya  kutumiwa katika huduma zilizokuwa zikitolewa na mabenki.Baadhi ya huduma hizo ni kama vile  kufanya mihamala kwa kushirikiana na mabenki kupitia simu za mkononi ,kuweka akiba na ,mikopo midogo midogo.Huduma hii imekuwa mkombozi kwa wanawake wengi nchini Tanzania ambapo imewawezesha kupata mitaji ya kuendesha biashara zao  ambazo nyingi haziko  katika mfumo rasmi.

Kupitia matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu za mkononi, yamewezesha wanawake kufanya shughuli zao kwa ushirikiano mkubwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali. Mifumo hii imewezesha makundi ya wanawake kuweza kujiwekea akiba na kupata mikopo ya kuendeleza shughuli zao, pia wemeweza kuanzisha vikundi mbalimbali vya uzalishaji na wengi wao kuendelea kunufaika nchini kote.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaweza kujivunia kwa kuanzisha sheria na usimamizi ambazo zimefanikisha watanzania wengi kuwa katika mfumo rasmi wa kifedha hasa kupitia huduma za simu za mkononi ambazo zimefanikisha suala hili haraka na kuwafikia wananchi nchini kote.

Kama nchi tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuleta mapinduzi ya kuwawezesha wananchi wengi kuingia katika mfumo rasmi wa kifedha. Mchango mkubwa wa kuleta mapinduzi hayo umewezeshwa na kuwepo huduma za kifedha kupitia simu za mkononi ambazo zinatolewa na makampuni yanayotoa huduma za simu za mkononi nchini.

 

Makala hii imetayarishwa na Vodacom Foundation Tanzania

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter