Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Zingatia misingi hii kufanikiwa

Zingatia misingi hii kufanikiwa

0 comment 115 views

Mabadiliko ni jambo la kawaida kwenye ulimwengu wa biashara hivi sasa hivyo kama mjasiriamali, unaweza kujikuta upo katika wakati mgumu hata kama ulikuwa na mpango wa kukuongoza katika biashara yako. Ni muhimu kusimamia malengo uliyojiwekea ili kufika mbali.

Hata kama una mpango madhubiti wa biashara, ni muhimu kuzingatia misingi ifuatayo ili kufanikiwa kwenye sekta hii:

Fahamu washindani wako

Kama mjasiriamali, ni vizuri kuwatambua washindani wako. Mbali na kuwatambua, unapaswa kujua bidhaa au huduma inayotolewa. Ufahamu huu utakusaidia kujipanga na kuhakikisha kuwa, huduma au bidhaa yako ipo katika nafasi nzuri zaidi sokoni. Tumia udhaifu walionao washindani wajo kuimarisha huduma na kuwavutia zaidi wateja.

Bana matumizi hata kama biashara inafanya vizuri

Wajasiriamali wengi hujisahau pindi tu biashara inapokubali sokoni na kuingiza faida. Ni vizuri kuendesha masiha yako kwa bajeti na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima. Endapo utaweka akiba, unaweza kustahimili changamoto zozote pindi zinapojitokeza na hivyo biashara itaendelea kubaki imara.

Tafiti bidhaa na huduma mpya

Ili kuwa katika nafasi nzuri, ni vizuri kufahamu na kuelewa bidhaa pamoja na huduma ambazo zinaweza kusaidia au kuinua biashara yako. Usiwe mtu ambaye hapendi kujifunza. Jenga mazoea ya kufanya utafiti ili kufahamu njia mbalimbali ambazo unaweza kutoa huduma bora zaidi.

Epuka tamaa ya soko kubwa ambalo lipo nje ya uwezo wako

Ikiwa bado upo hatua za mwanzo, ni muhimu kulega wateja ambao unaweza kuwahudumia na kadri unavyozidi kukua unaweza kupanua wigo wa biashara yako kidogo kidogo. Wafanyabiashara wengi hukwama kwani wanalenga kufanya mambo makubwa wakati uwezo wao bado ni mdogo.

Sikiliza maoni ya wateja

Mjasiriamali anayo nafasi kubwa ya kuimarisha biashara yake kwa kusikiliza kero, maoni na ushauri moja kwa moja kutoka kwa wateja na kuchukua hatua stahiki ili kuboresha huduma. Ni muhimu kuwasikiliza wateja wako na kuyafanyia kazi maoni yao.

Kubali mabadiliko

Katika ulimwengu wa biashara, ni vigumu sana kuepuka mabadiliko. Kama mjasiriamali, unatakiwa kujiandaa kukabiliana na mabadiliko na kubadilisha mwenendo wa biashara yako. Usikubali kuachwa nyuma. Ifahamike kuwa vile ulivyoanza biashara yako sio itakavyokuwa miaka 10 au 15 ijayo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter