Home KILIMO Biashara ya Mboga Mboga (Mchicha)

Biashara ya Mboga Mboga (Mchicha)

0 comment 381 views

Wakati tunaanza kupanda ngazi za mlima wa  malengo yetu ya mwaka 2020, najua kuna wengine bado wapo kwenye fikra ya biashara gani wanaweza kuifanya kwa mtaji mdogo.

Je, ulishawahi kufikiria kuhusu Biashara ya mboga mboga.

Hii ni biashara ambayo unaweza kuifanya na ikakusaidia kuelekea kutimiza malengo yako mwaka huu.  Kuna njia mbili unazoweza kutumia kufanya biashara hii.

  • Kulima Bustani yako na kuuza mwenyewe.
  • Kununua kutoka kwa wakulima wengine na kuuza.

Leo tutazungumzia njia mojawapo ambayo ni kulima Bustani na kuuza mwenyewe.

Kwa kawaida mazao ya mbogamboga huwa yanatumia muda mfupi sana kulima hadi kuvunwa.

Mfano unaweza kuanza kwa kulima mchicha.

Mchicha ni moja ya aina mboga za majani ambayo ustawi maeneo mengi ya Tanzania na ustawi kwenye eneo lenye rutuba lisilotuamisha maji.

Eneo unalopanda mchicha zingatia pawe na upatikanaji wa maji karibu ili kurahisisha umwagiliaji na kufanya mchicha wako ukue vizuri na upendeze machoni kwa wateja wako.

Mchicha unakuwa tayari kuvunwa wiki 2 hadi 4 tangu kupandwa.

Unaweza kuvunwa kwa kungoa au kukata majani ya juu na kuacha mashina yakiendelea kuchipua upya, huku ukiendelea kumwagilia bustani yako.

Kama mchicha utatunzwa vizuri unaweza kuendelea kuvunwa kwa muda wa miezi 3 au zaidi.

Mchicha unaweza kuusambaza majumbani, kwenye migahawa na hata kwenye mahoteli.

Zingatia usafi katika mchakato mzima tangu upandaji adi unaposambaza kwa ajili ya kuuza, hii itakurahisishia kujiweka tofauti na wasambazaji wengine.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter