Home BIASHARAUWEKEZAJI Uchumi endelevu wa bahari kunufaisha Tanzania

Uchumi endelevu wa bahari kunufaisha Tanzania

0 comment 23 views

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili na Utalii, Uvuvi na Mifugo Zanzibar, Dk. Islam Seif Salum ameeleza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa Tanzania kama taifa kunufaika na fursa mbalimbali za uchumi endelevu wa bahari katika sekta za uvuvi, utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi na vilevile katika sekta ya utalii.

“Tuko hapa kujadiliana na kuweka mikakati ya pamoja kama nchi katika kuelekea mkutano mkubwa wa masuala ya kunufaika na rasilimali za uvivu katika bahari, mito, maziwa na mabwawa, dhana hii ni mpya hapa nchini kwetu ingawa tunatekeleza kwa kiwango kidogo”. Amesema Dk. Salum.

Naibu Katibu huyo amesema mkutano huo utatengeneza fursa zaidi za kuwekeza katika rasilimali za baharini ili kufanikisha azma ya kukuza uchumi na kuwezesha Tanzania ya viwanda.

Naye Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Emelda Teikwa amesema dhana nzima ya ‘Blue Economy’ ni mpya kwa watanzania lakini umuhimu wake katika uchumi ni mkubwa.

“Tunaangalia namna ambavyo uchumi wa bahari unaweza kuchangia katika kukuza pato la taifa, kwa kuwa na uvuvi endelevu na kukuza sekta ya utalii”. Amesema Teikwa.

Tanzania ni moja kati ya nchi zitakazoshiriki katika mkutano mkubwa wa uchumi endelevu wa bahari (Sustainable Blue Economy) utakaofanyika Kenya mwishoni mwa mwezi huu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter