Home KILIMO Dk. Mahenge awataka wakulima kufikiri nje ya boksi

Dk. Mahenge awataka wakulima kufikiri nje ya boksi

0 comment 99 views

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Bilinith Mahenge amewataka wakulima kuacha kuishi kwa mazoea kwa kulima mazao ambayo hayawaletei faida  na kuchangamkia fursa ya mazao yanayostawi zaidi mkoani humo kama  mtama,uwele,mpunga,karanga,muhogo,alizeti, na zabibu ili kuongeza pato lao na la taifa.

Muheshimiwa huyo amesema katika mazao matano ya kimkakati kutokana na serikali mazao mawili yanastawi vizuri mkoani humo, mazao hayo ameyataja kuwa ni Pamba na Alizeti. Pia amewataka wakulima kupunguza kulima mazao yanayotaka mvua kubwa kama mahindi na kushughulika zaidi na mazao yanayoitaji mvua ya kawaida na yenye faida zaidi.

Dk.Mahenge ametaja Zabibu kuwa moja ya zao lenye soko kubwa mkoani humo na hivyo kuwataka wakulima wa zao hilo kulima kwa wingi ili waweze kufaidika zaidi na kuleta maendeleo nchini.

Aidha, Mkuu huyo amekua akipata ushirikiano kutoka kwa wakuu wa wilaya wa mkoani humo ili  kuhakikisha kuwa kila mkulima  anaweza kulima ekari mbili na kuendelea mazao ya chakula na biashara ili aweze kujipatia maendeleo ya kiuchumi na kifamilia.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter