Home KILIMO Fahamu haya kuhusu muhogo

Fahamu haya kuhusu muhogo

0 comment 154 views

Muhogo ni moja ya mazao ambayo yanalimwa sana hasa kutokana na tabia yake ya kuvumilia hali ya ukame. Kwa Tanzania wakulima wengi hasa wadogo hupendelea kuchanganya zao hili na mazao mengine kama maharage, kunde, mbaazi, njugu mawe n.k.

Hivyo haya ni baadhi ya mambo ambayo unaweza kuwa hufahamu kuhusu muhogo:

  • Muhogo unaweza kuchukua hadi miezi 18 kuwa tayari kwa ajili ya mavuno, ambapo inahitaji miezi 8 na kuendelea kukua katika hali yenye joto na hufanya vizuri zaidi ikikua kwenye jua,
  • Muhogo unaweza kuvumilia hali ya ukame na kuweza kukua kwenye udongo usio na rutuba. Kawaida, sio rahisi kwa muhogo kushambuliwa na wadudu na magonjwa ya mimea.
  • Muhogo unaweza kuhifadhiwa chini ya ardhi kwa miaka miwili bila kuoza.
  • Mihogo unajulikana kwa majina mengi ikiwa ni pamoja na yucca, manioc, mandioca, mizizi ya yucca, casaba, na tapioca.
  • Watu wengi hupendelea kula muhogo kwa sababu ni rafiki kwa afya na chakula kwa ujumla
  • Muhogo hutengenezwa katika njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchemsha, kuoka, kukaanga, kuchoma, na kwa Tanzania watu hutengeneza unga wa muhogo na kupika ugali wa muhogo.
  • Kuna aina mbili za muhogo – muhogo mtamu na mchungu. Muhogo mchungu hutumika kwenye mikate na keki.
  • Muhogo una kalori nyingi pamoja na wanga.
  • Shirika la Kansa huko Marekani linawaonya watu wenye aleji na mipira ya Latex kuwa makini na muhogo kwani wanaweza kupata aleji ikiwa watatumia mihogo
  • Inashauriwa kutokula muhogo ukiwa mbichi, kwa sababu ndani yake kuna kitu kinaitwa cyanide ambacho si nzuri kwa afya ya binadamu na kinaweza kupelekea binadamu kupata matatizo ya kutembea, magonjwa ya chronic pancreatitis . Ndio maana taasisi ya The Bill and Melinda Gates Foundation inasaidia kuzalisha mihogo yenye cyanide kidogo.

Hivyo baada ya kujua hayo jambo la kuzingatia ukiwa unatengeneza muhogo ni kwanza kuosha na kumenya vizuri, na kwa ajili ya mambo ya kiafya unashauriwa kuuoweka muhogo, kukausha na baada ya hapo kupika vile unavyotaka. Maeneo mengi yenye ukame na njaa hulima zao hili kwa sababu ya ustahimili wake mkubwa wa udongo mbaya na kuhitaji maji machache ili kukua.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter