Mkuu wa mkoa wa tabora,Aggrey Mwanri ameagiza kukamtwa kwa wakulima mbalimbali ambao wamelangua mbolea kutoka vyama vya ushirika na kuiuza kwa maslahi binafsi.
Wakulima hao wasio waaminifu hukopa mbolea ya kukuzia tumbaku kwa sh.82000 na wao huiuza kwa magendo kwa walanguzi kwa bei ya sh.50000.
Mkuu huyo wa mkoa mwenye misamiati yenye kufurahisha alitoa agizo hilo baada ya kupokea ripoti kutoka kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tabora Said Ntahondi ambayo ilibainisha uwepo wa biashara hiyo ya magendo ambayo mwishowe humfanya mkulima kubeba mzigo mkubwa wa madeni ambao haulipiki hivyo kuviathiri vyama vyao vya ushirika.
Mwanri alisisitiza hakuna mkulima anayeruhusiwa kuuza kwa mwingine aina yeyote ya pembejeo alizokopeshwa hasa mbolea kwani kosa kisheria na muuzaji na mnunuzi wanapaswa wachukuliwe hatua na kufikishwa mahakamani.
Pia mwanri alimaarufu kama “mzee wa fyekyelea mbali” aliwaasa wakulima hao kulipa kodi ili kuongeza mapato katika halmashauri zao.