Home KILIMO Kilimo cha korosho kuwa zao lingine la biashara Sikonge

Kilimo cha korosho kuwa zao lingine la biashara Sikonge

0 comment 202 views
Na Mwandishi wetu

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Simon Ngatunga amesema wilaya hiyo inatarajia kuanzisha kilimo cha korosho kama zao la biashara ambalo litaungana na zao la tumbaku ikiwa ni hatua mojawapo ya kuandaa malighafi kwa ajili ya viwanda. Mkurugenzi huyo amesema uwepo wa zao lingine la biashara pia unatoa fursa nzuri kwa wakazi wa wilaya hiyo kujiingizia kipato.

Ngatunga ametoa maelezo hayo wakati akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambapo ameeleza kuwa barua tayari imewasilishwa kwa bodi ya korosho nchi ili wapatiwe miche ya mikorosho ambayo itapandwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo. Ameongeza kuwa kilimo hicho mbali na kuwa chanzo cha malighafi viwandani pia kitasaidia kupunguza uharibifu wa misitu uliopo hivi sasa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka viongozi katika halmashauri zote nane mkoani humo kusisitiza juu ya kilimo cha alizeti, korosho na pamba na kusema lengo kubwa ni kuwa na malighafi ya kutosha kwa ajili ya viwanda kwani ardhi ya Tabora inakubali mazao mbalimbali hivyo wananchi watumie fursa hiyo kujiinua kiuchumi kwani kwa kufanya hivyo wanainua pia mapato cha halmashauri

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter