Home KILIMOKILIMO UFUNDI Mradi wa Dola za Marekani milioni 154.06 kusaidia wakulima 4,800,000

Mradi wa Dola za Marekani milioni 154.06 kusaidia wakulima 4,800,000

0 comment 78 views

Wizara ya Kilimo imetambulisha mradi wenye gharama za Dola za Marekani milioni 154.06 na walengwa wa moja kwa moja ni wakulima 4,800,000 wakiwemo wanawake na vijana waliopo katika mnyororo wa thamani ya mazao ya ngano, alizeti na mpunga.

Lengo la mradi huo niujulikanao kama Mradi wa Kusaidia Pembejeo za Kilimo Tanzania (TAISP) ni kuongeza tija kwenye kilimo na kuimarisha usalama wa chakula nchini.

Zoezi la kutambulisho mradi huo limefanyika Oktoba 30, 2023 mkoani Mwanza katika Ukumbi wa Mikutano wa TMDA.

Mratibu wa mradi wa TAISP Kissa Chawe, ameeleza kuwa hatua hiyo imelenga kuongeza uzalishaji wa chakula wa ndani na kuimarisha ustahimilivu wa mifumo ya chakula.

Amesema utararibu huo unalenga kupunguza hatari za muda mfupi na mrefu kutokana na athari za vita vya Ukraine na Urusi pamoja na mabadiliko ya tabianchi.

Mradi huo wa TAISP unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, Shirika la Maendeleo la Japan na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mradi huo w amiaka mitatu, utatekelezwa katika mikoa 14 kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter