Home KILIMO Makamu wa Rais kufungua maonyesho ya Nanenane Simiyu

Makamu wa Rais kufungua maonyesho ya Nanenane Simiyu

0 comment 90 views

Kwa kutambua mchango wa Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi  katika kuinua uchumi wa Tanzania, Wakuu wa Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga kwa kushirikiana na Mawaziri wenye dhamana ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji wanawakaribisha Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na Wadau wengine kwenye maonesho na maadhimisho ya sikukuu ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia tarehe 28/07/2019 na kilele chake kuwa tarehe 08/08/2019.

Ufunguzi rasmi wa Maonyesho hayo utafanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan siku ya tarehe 01/08/2019. Kauli mbiu ya Nanenane mwaka huu ni “Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa Uchumi wa Nchi”.

Wakati wa maadhimisho hayo, tarehe 03/08/2019 itakuwa siku ya “Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP ll)” Mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kasimu Majaliwa Majaliwa, siku ambayo wananchi watajenga uelewa zaidi kuhusu utekelejazi wa “Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili’

Mgeni Rasmi siku ya kilele ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Kutakuwa pia na mafunzo ya nadharia na vitendo kwa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi ili kuongeza uzalishaji na tija. Sambamba na hiyo  kutakuwa na kongamano kuhusu namna bora ya kuendesha kilimo biashara, teknolojia mpya, masoko na mitaji.

KARIBUNI KANDA YA ZIWA MASHARIKI ili kuona fursa mbalimbali zitakazomwezesha mwananchi kuinua uchumi wake binafsi na Taifa kwa ujumla.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter