Sekta ya kilimo cha mboga mboga na matunda ni moja ya sekta zinazokua kwa haraka kwa mwaka. Sekta hii inakua kwa kati ya asilimia 7 mpaka 11 ukilinganisha na ukuaji wa sekta ya kilimo ambayo ni asilimia 4 hadi tano.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema sekta hii inatoa ajira za moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja kwa watu takriban I milioni 6.5.
Sekta hii inatajwa kuwa na mvuto kwa makundi ya wanawake na vijana hivyo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi jumuishi. Pia ina fursa ya kukabiliana na utapiamlo.
Waziri Bashe alitaja changamoto kwenye kilimo ikiwemo bei ya mbolea katika soko la dunia ambapo alisema imepanda kwa zaidi ya asilimia 300.