Home KILIMO Wakulima mbaazi walilia soko

Wakulima mbaazi walilia soko

0 comment 118 views

Kufuatia India kuacha kununua zao la mbaazi nchini kwa sababu ya kuwa na akiba ya kutosha, soko la mbaazi limeshuka sana hali iliyowafanya wakulima wa Halmashauri ya Mji wa Babati kuiomba serikali kuwatafutia soko nje ya nchi ili waweze kujikwamua kimaisha na kuendelea kuchangia katika pato la taifa.

Mkulima wa zao hilo Veronica Aloyce, amewaambia waandishi wa habari kuwa mwaka 2014/16 walikuwa wakiuza zao hilo Sh. 2,000 kwa kilo lakini bei hiyo imeshuka hadi Shilingi 300 kwa kilo jambo ambalo linawakosesha matumaini ya kutaka kulima hekari nyingi.

“Mimi ni mama wa watoto sita kwa msimu huu nimelima zao la mbaazi hekari tano tu kwa sababu hatuna uhakika wa kupata soko pindi mazao yetu yatakapo komaa”. Amesema Mkulima huyo.

Mwenyekiti wa Mtaa, Gendi Barazani  Benard Daat, amesema kuwa zao la mbaazi halina soko maalumu na ubora wa zao hilo ndio namna pekee mkulima ataweza kupata soko. Pia ameongeza kuwa kuna mabadiliko makubwa katika soko la zao hilo ambapo zamani wakulima waliweza kuuza zao hilo kwa Shilingi 300,000 kwa gunia hadi 350,000 lakini sasa wakulima wanauza gunia moja kwa Shilingi 80,000.

Kwa upande wake, Diwani wa Viti Maalumu Halmashauri ya babati mjini Rose Muryang, amewataka wakulima hao kuunda umoja kwa kupitia vyama na kumtafuta mnunuzi wa zao hilo kutoka kampuni ya Export Trading Group (ETG).

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter