Naibu Waziri wa Kilimo Mary Mwanjelwa amesema serikali imeanza uchunguzi wa kubaini wale waliohusika na kupelekwa kwa korosho zilizochanganywa na mawe nje ya nchi na kauli itatolewa mara baada ya uchunguzi huo kukamilika. Waziri Manjelwa amesema hayo bungeni Dodoma na ameongeza kuwa serikali inawachunguza wote walioripotiwa katika taarifa ya timu ya uchunguzi na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wale watakaobainika kuruhusu korosho hizo kusafiri. Serikali pia imetoa wito kwa Bodi ya Korosho nchini, Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi Ghalani, Mamlaka ya serikali za mitaa pamoja na Tume ya Maendeleo ya Ushirika kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano.
110