Kampuni ya simu ya Vodacom imetoa mafunzo ya huduma ya kwanza kwa wafanyakazi wake katika jitihada za kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wao wakiwa nyumbani na ofisini.
Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa siku mbili na kampuni ya zima moto na uokoaji ya Knight Support.

Mwalimu wa mafunzo ya huduma ya kwanza kutoka Knight Support Company, Bw Adam akitoa mafunzo hayo kwa wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom katika semina ya siku mbili iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo wiki hii jijini Dar es Salaam. Kampuni ya Vodacom hutoa mafunzo mbalimbali ya uokoaji kwa wafanyakazi wake na wafanyakazi wa majumbani kwao ili kuwawezesha kukabiliana na ajali mbalimbali ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wake.

Mfanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc Neema Mgombelo, akionyesha mfano wa jinsi ya kumtambua mgonjwa aliezimia katika semina ya mafunzo ya huduma ya kwanza, iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kampuni ya Vodacom hutoa mafunzo mbalimbali ya uokoaji kwa wafanyakazi wake na wafanyakazi wa majumbani kwao ili kuwawezesha kukabiliana na ajali mbalimbali ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wake. Kushoto ni Mwalimu wa mafunzo hayo Bw Adam kutoka kampuni ya Knight Support Company.