Siku ya alhamis tarehe 11/10/18 inabaki kuwa siku ya kukumbukwa na Watanzania wengi kufuatia tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara mashuhuri nchini Mohamed Dewji “Mo”,aliyetekwa alfajiri wakati akiingia hotelini kufanya mazoezi.
Mo Dewji, tajiri kijana barani afrika huku akishika nafasi ya 17 kwa afrika katika orodha ya utajiri kwa ujumla.Mfanyabiashara huyo maarufu aliyezaliwa mwaka 1975 ni mkurugenzi mkuu wa makampuni ya Metl Group ambaye kwa mujibu wa mtandao maarufu duniani wa wikipedia ana utajiri wa dola za kimarekani 1.5 bilioni.
Pia Mo anachangia pato la taifa kwa takribani 3.5% huku akiwa ameajiri watu takribani 20000 katika makampuni yake tofauti tofauti.
Pesatu.com ilichukua maoni ya baadhi ya Watanzania kama kutekwa kwa mfanyabiashara huyu kunaathiri sekta ya utalii na uchumi kwa ujumla?ungana nasi pia unaweza kuacha maoni yako hapo chini.