• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Sunday, June 26, 2022
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Sera ya diplomasia ya uchumi inavyoleta mageuzi ya uwekezaji

Patricia Richard by Patricia Richard
October 19, 2018
in UWEKEZAJI
0
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga

Share on FacebookShare on Twitter

Na. Immaculate Makilika

MAELEZO

DAR ES SALAAM

KATIKA miaka ya 1960 hadi 1980 malengo ya ziada katika Sera ya mambo ya nje ya Tanzania yalikuwa ni ukombozi wa Bara la Afrika kutoka kwa makucha ya ukoloni na ubaguzi wa rangi.

Baada ya kukamilisha juhudi hizo, Tanzania ilifanya mageuzi makubwa katika Sera ya Mambo ya Nje iliyoweka msisitizo wa diplomasia ya uchumi ili kusukuma maendeleo ya Taifa.

Diplomasia ya uchumi ni msisitizo wa Sera ya Mambo ya Nje yenye mikakati, malengo, mbinu na maarifa yanayoelekeza taifa kupata na kuvuna rasilimali na utaalam kutoka jumuiya ya mataifa ili kuleta na kuchochea maendeleo ya taifa husika.

Mwaka 2001 Tanzania ilipitisha sera hiyo ili kuharakisha maendeleo hasa katika mageuzi ya kiuchumi kupitia uwekezaji, ambapo katika mwendelezo huo Serikali ya Awamu hii ya Tano, inayoongozwa na  Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeongeza kasi ya utekelezaji wa sera ili kuifanya Tanzania kufikia nchi ya kipato cha uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Azma hii inamaanisha kuwa diplomasia ya uchumi lazima iongeze mkakati wa Diplomasia wa viwanda ili kutekeleza maono na mawazo ya Rais Dkt. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kupitia malighafi za mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahriki  kwa mwaka 2018/2019, Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga anasema kuwa sera ya diplomasia ya uchumi imeweka vipaumbele katika uwekezaji, miundombinu ikiwa ni pamoja na nishati, biashara na masoko ya bidhaa kutoka viwandani, kilimo, utalii na madini

Aidha, Balozi Mahiga anasema kuwa Serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali ili kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2025, ambapo hivi karibuni Wizara hiyo imeratibu maonesho ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania, yaliyofanyika  mjini Nairobi nchini Kenya.

“Katika maonesho hayo ya kipekee kuwahi kufanywa na Tanzania huko nchini Kenya jumla ya kampuni 27 zinazozalisha bidhaa za viwandani kutoka Tanzania zilishiriki ili kutangaza bidhaa na kuvutia utalii, ambapo yaliyotoa fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kutafuta masoko nchini humo  na kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili” anasema Waziri Mahiga.

Aidha, Balozi Mahiga anasema kupitia sera ya diplomasia ya uchumi, Serikali za Tanzania na Misri, zimeratibu  majadiliano ya pamoja hatua iliyosaidia kuondoleana ushuru wa forodha kwa kiwango cha asilimia 100, huku Tanzania ikiondoa  ushuru kwa kiwango cha asilimia 96.89, ambapo kiwango kilichosalia kitaondolewa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

ADVERTISEMENT

Katika kuchagiza sera hiyo, Dkt. Mahiga anasema mwezi Februari, mwaka huu, Serikali za Tanzania na Korea Kusini ziliandaa kongamano la biashara na uwekezaji kati ya mataifa hayo mawili, kufuatia mazungumzo baina ya viongozi wa kampuni ya Hyundai na Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC).

Aidha, Balozi Mahiga anasema aliwataka wadau wanaosimamia masuala ya biashara na uwekezaji kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji wanaoonesha nia ya kuwekeza nchini.

Tags: biasharaDkt. Augustine MahigamaendeleoTICuchumiviwanda
Patricia Richard

Patricia Richard

Next Post

Wiki moja tangu kutekwa kwa Mo Dewji

Discussion about this post

Habari Mpya

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

June 24, 2022

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

June 23, 2022

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

June 23, 2022

Turkish Airlines yarejesha safari zake KIA

June 22, 2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akizungumza katika warsha ya viongozi wa Serikali wa mkoa na Bank ya NMB.

Benki ya NMB yapongezwa

June 22, 2022

Rais Samia azindua taasisi Zanzibar

June 20, 2022

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

by Pesatu Reporter
June 24, 2022
0

Miamala ya fedha kwa njia ya simu imechangia kuongezeka kwa pato la Taifa kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi kufikia...

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

by Pesatu Reporter
June 23, 2022
0

Mapendekezo yamepitishwa kwa kila Mtanzania kuwa na bima ya afya. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) leo 23...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2022 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In