Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation wakishirikiana na Doris Mollel Foundation leo wamechangia vifaa tiba vyenye thamani ya shilling milioni 25 katika hospitali iliyopo kwenye kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma ili kuongeza juhudi za kuhakikisha watoto wanaozaliwa njiti katika kambi hiyo wanaishi. Hospitali hiyo hutoa huduma kwa Wakimbizi waishio kambini hapo na wale wa kambi jirani ya Mtendeli lakini pia wanajamii wanaoishi maeneo jirani na kambi hizo.
Takwimu zinaonyesha kwamba kila mwaka watoto millioni 15 huzaliwa kabla ya wakati yaani njiti kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania ambapo watoto milioni 1 hufariki kwa kukosa huduma muhimu. Vodacom Tanzania Foundation imekuwa mstari wa mbele kuchangia vifaa tiba katika vituo vya afya na hospitali hapa nchini ilikuokoa maisha ya watoto njiti.
“Watoto njiti wana nafasi kubwa yakukua na kuwa na afya nzuri bila ulemavu endapo watapata msaada wa vifaa na usimamizi wa afya kuzingatiwa na ndio maana sisi kama Vodacom Tanzania Foundation tunafuraha sana kuwa sehemu ya wanaochangia kuhakikisha watoto njiti nchini wanaishi” alisema Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mahusiano Bi Jacquiline Materu huku akiongeza kwamba Vodacom Tanzania Foundation imejikita katika kuboreshahuduma za afya na elimu kwa Wanawake pamoja na watoto nchini Tanzania.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya serikali mwakilishi wa Katibu mkuu wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto (anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) Dr John Jingu, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu Titus Mguha alizishukuru taasisi za Vodacom Tanzania Foundation na Doris Mollel kwa kuunga juhudi za serikali za kuokoa maisha ya watoto “Msaada huu umekuja ndani ya muda muafaka wakati ambapo serikali imezindua kampeni ya Jiongeze Tuwavushe salama kuhamasisha watu na Taasisi mbalimbali kupigania kupunguza vifo vya akina mama na watoto. Ninafuraha kubwa kuona muungano huu wa Vodacom Tanzania Foundation na Doris Mollel Foundation ukifanya kazi kuboresha afya ya watoto na mama katika kambi hii,”alisema.
Kwa upande wake, mratibu wa afya katika kambi ya Nyarugusu Dr Athumani Juma alisema hospitali hiyo imekuwa na changamoto yakusaidia maisha ya watoto njiti wanaozaliwa hapo hospitalini.
“Tumefanikiwa kukarabati wodi ya watoto njiti lakini tulikuwa na changamoto ya vifaa hivyo tunashukuru sana kwa mchango huu wa vifaa vya kuokoa maisha yawatoto njiti wanaozaliwa hospitalini hapa na tunaahidi uangalizi wa karibu”
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na vifaa vya oksijeni (Oxygen concentrator) ambavyo vitasaidia
Watoto njiti kupumua, thermometers 10, 4 weighing scales for infants, 40 branded bed sheets, baby warmer, 3 suction machines, ambu bag with facemasks for infants, 1000 feeding tubes, phototherapy machine, na vitanda vitatu vya watoto.