Home VIWANDAMIUNDOMBINU Miradi ya bilioni mbili yazinduliwa Mwanza

Miradi ya bilioni mbili yazinduliwa Mwanza

0 comment 101 views
Na Mwandishi wetu

Akiwa mkoani Mwanza, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Amour Hamad Amour amezindua na kuweka jiwe la msingi kwenye miradi nane ya maendeleo wilayani Misumbwi ambayo thamani yake inafikia Sh. 2.2 bilioni.

Miongoni mwa miradi hiyo ni kiwanda cha kuchakata gesi ya matumizi ya nyumbani, Shamba la kuku la Prime Farm Ltd, barabara ya Lubuga-Mwaniko hadi Mondo na mengineyo. Amour pia ametoa shukrani kwa Rais Magufuli kuendelea kuwapa vijana fursa ya kuwatumikia watanzania.

Baada ya kuzindua miradi hiyo, kiongozi huyo amesema ameshuhudia miradi mbalimbali inayoongozwa na vijana ikiwa katika ubora huku vijana hao wakijituma kama serikali ya awamu ya tano inavyotaka huku akisisitiza kuwa Rais Magufuli hakukosea kuwateua vijana katika nafasi hizo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda pamoja na Mkurugenzi wake Eliurd Mwaiteleke wamepongezwa kutokana na jitihada zao katika kufanikisha sera ya viwanda na kuunga mkono maagizo ya Rais Magufuli.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter