Home KILIMO Wakulima waache kilimo cha mazoea

Wakulima waache kilimo cha mazoea

0 comment 67 views
Na Mwandishi wetu

Wakulima nchini wameshauriwa kuachana na kilimo cha mazoea na kuanza kutumia kilimo hifadhi ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kuweza kuingia katika masoko ya mfumo rasmi ili wapate kunufaika na kuzalisha kwa tija.

Mratibu wa Mradi wa African Conservation Tillage Network (ACTN) Abiud Gamba amesema mradi huo unafanya kazi ya kuelimisha wakulima kutumia teknolojia katika kilimo chao ili kuboresha na kuimarisha rutuba ya udongo, na kwamba mradi huo umelenga kufikia wakulima 45,000 na umefanya kazi katika wilaya nne za Kilolo mkoani Iringa, Namtumbo na Songea vijijini pamoja na Ludewa mkoani Njombe.

Mpaka hivi sasa madarasa shamba 200 yamekwishatolewa kwa maofisa ugani juu ya kilimo hifadhi huku Gamba ameshauri serikali iendelee kushirikiana nao ili waendelee na kazi hii ya kuelimisha maofisa hawa juu ya kilimo hifadhi. Katika ufunguzi wa mradi huo, Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Kilolo Moses Logan alisema mradi huu upo kwa ajili ya kuangalia rutuba ya udongo kwa kufunika udongo kupitia masalia ya mazao badala ya kuyachoma moto.

Logan aliongeza pia kuwa, mradi huu ulitekelezwa na wadau wanne ambao ni ACTN, CRDB Pass, Briten pamoja na Rudi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter