Home VIWANDAMIUNDOMBINU Flyover yazalisha ajira 700

Flyover yazalisha ajira 700

0 comment 92 views

Mwakilishi Mkuu wa shirika la maendeleo la kimataifa la Japan (JICA), ofisi ya Tanzania, Toshio Nagase amesema daraja la juu la Tazara maarufu kama flyover limezalisha ajira zaidi ya 700 kwa watanzania mbalimbali. Baadhi ya kada zilizonufaika na mradi huo ni pamoja na ufungaji wa vyuma kipindi cha ujenzi, kingo za daraja, uwekaji wa taa, ubebaji zege pamoja na uendeshaji wa mitambo ya kuchanganyia zege.

Nagase amesema hayo wakati akizungumzia miradi ya shirika hilo na kuongeza kuwa, asilimia kubwa ya walionufaika na ajira ni watanzania huku akikiri uwepo wa wataalamu kadhaa kutoka Japan ambao walikuwa na jukumu la kusimamia ujenzi huo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwakilishi huyo, katika ajira hizo 700, wamo vibarua na waajiriwa kwenye kazi za kitaalamu ambao amedai, wameonyesha uwezo mkubwa wa kujituma.

“Vijana hao wametusaidia katika ujenzi wa daraja hili ambalo limegharimu Sh. 100 bilioni na wameshiriki kikamilifu katika ujenzi wake, wamekuwa wakifanya kazi kwa muda wote kuanzia muda wa kazi na hadi wa kuondoka bila ya kuleta usumbufu na wamesaidia kuandika historia hii ya kuwa mradi ulioanza hadi kumalizika bila ya kuwapo kwa ajali kwa wafanyakazi na mradi”. Amesema Nagase.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter